aleluya, kwa kweli tunamshukuru MUNGU wetu MKUU BABA yetu katika YESU KRISTO BWANA wetu na katika Uwepo wa ROHO MTAKATIFU kwa Neema, Rehema,Baraka na UPENDO MKUU aliotupatia katika Mwezi wetu wa Kufunga na Kuomba, Mwezi wa Tano (May/2014) uliopita, kweli tuliona MAMBO MAKUU, Tuliona KIBALI, Oooh MUNGU Anatupenda WANAWE, Nasi tutazidi KUMPENDA na KUMPENDA na KUMPENDA na tutampinga na kumkataa shetani ibilisi mlaaniwa. Sasa Wana wa MUNGU kazi ni mbele kwa mbele " KUMPINGA shetani na KUMKATAA, kwani tunayo NGUVU na MAMLAKA ya Kukanyaga nyoka na ng'e na kushinda nguvu zote za yule adui; na wala hakuna kitu cho chote kitakachoweza kutudhuru" Usicheze naye, usicheke naye, atakuabisha, atakurudisha nyuma, atakupotezea muda, atakufanya uchelewe kupokea Matazimio yako; Kuwa na HASIRA YA MUNGU, kuwa na WIVU WA MUNGU, Usirudi Nyuma tena Mwana wa MUNGU. Na wewe ambaye bado hujampokea YESU, njoo sasa achana na Maisha ya Mateso, ya kuburudhwa na shetani, anakufanya Uteseke, uhangaike, usiwe na Amani na Furaha katika maisha yako, matatizo mateso hayaondoki kwako, magonjwa, misiba... AMUA SASA, Umpokee YESU, Njoo kwa YESU sasa. Mbarikiwe.

Comments