YESU anakupenda! kama mimi alinipenda na akaniambia nimtumikie na mimi nikasema nina dhambi akaniuliza nani kakwambia una dhambi?.….mnajijua kwamba mna dhambi basi ujue YESU anakupenda sana pamoja na dhambi zako. Huu ni Mwaka wa Kibali inakupasa kutafuta kondoo na kuwa kama Paulo, aliwavuna wasomi tamani na wewe upate mtu wa kumlea katika wokovu mpaka asimame. YESU alifuatwa na watu wengi sana lakini alitembelea nyumba chache za wasomi, kwahiyo tunaenda kulingana na elimu yako. Kila mtu avune onyesha umekuwa mwanzo, Biblia inasema jaribuni mambo yote. Onyesha ushuhuda wako uwe wa thamani na onyesha kwamba umekuwa Kiroho, kama unakaa Mikocheni gonga geti nyumba ya pili ambayo imefungwa geti kama la kwako fanya kitu kitakachofanya MUNGU ajue una akili. Kwani tuna Roho ya Ufahamu basi wote tuwe na akili ya MUNGU tunatakiwa kuona nani ameelewa, embu panda kiwango kidogo katika utumishi wako( try to make a standard )..... (Sehemu ya Mahubiri ya Ibada ya Jana tarehe 25.5.2014 Efatha Ministry Mwenge na Mtuymishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira) Ibada zilikuwa nzuri sana katika Makanisa yote ya Efatha Ministry ndani na nje ya Tanzazania, maana zile ROHO ZA SABA na NGUVU YA MUNGU Imo ndani yeu,Ooooh ASANTE YESU, Tunakupenda BWANA Haleluya.

Comments