UTUKUFU na UKUU na MAMLAKA ni kwa YEYE aliye BWANA na MUNGU wetu MKUU, SIFA na HESHIMA ni zake, Tunamuabudu Asubuhi hii na Kumtukuza tunamwambia BABA Asante, Asante kwa asubuhi hii njema na nzuri, yenye Rehema na Neema na Baraka tele, Wewe ni MUNGU wetu, Wewe ni BABA yetu Asante, TUNAKUPENDA MUNGU wetu, Tunakupenda, Wewe ni ALFA & OMEGA, MWANZO & MWISHO, Tunakutuza MUNGU wetu, Haleluya... Asubuhi njema imewadia na Wana Efatha tunakimbilia Madhabahuni mwa BWANA MUNGU wetu, Hemani mwa BWANA tayari kwa ajili ya Ibada yenye Utukufu wa MUNGU na MAFUNDISHO yenye Uwepo na Nguvu ya MUNGU, Tayari kwa ajili ya Upendo wa BWANA wetu YESU KRISTO kututoa Utotoni na Kutupeleka kwenye UWANA, WANA WA MUNGU, Haleluya; YESU YESU YESU TUNAKUPENDA BWANA, TUNAKUPENDA, Asante BWANA, Asante, Uwe nasi Siku ya Leo, Usimpite hata mmoja BWANA Haleluya, ROHO MTAKATIFU MUNGU Uwepo wako, Uongozi wako ndani yetu Ukatawale ili Tukapokee kile ambacho BABA kupitia Mtumishi wake Mwaminifu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira Amekusudia, Asante ROHO MTAKATIFU MUNGU Asante Tunakupenda, Amen. (Ibada hii italushwa Live kupitia kituo chetu cha Television TRENET via Satelite, pamoja na kwenye kingamuzi cha TING, na tutakuwa tunawaletea baadhi ya dokezo au matukio yatakayokuwa yanaendelea Ibadani hapa kwenye Page yetu ya Efatha Ministry, MUNGU Akawabariki, na muwe tayari kupokea kwa Moyo mmoja, Mbarikiwe.)

Comments