ROHO YA UFAHAMU Roho ya UFAHAMU inaenda pamoja na Roho ya HEKIMA. Inakupa kujua yaliyopita na yaliopo, inakusaidia usiishi kwa mazingira yanayokuzunguka au yaliyokuzunguka bali vile MUNGU anavyokuona, kupitia Ufahamu unaweza kujua juu ya familia yako na uzao wako. Unaweza tu ukazuia mambo yaliopo kwa kupitia Ufahamu, Hekima Ufahamu unakupa KUPONYEKA, kama umetoka katika jamii iliyopitia maumivu ili uweze KUPONYEKA unahitaji UFAHAMU. Rumi 1:28-29 Unapokosa Ufahamu MUNGU anakutelekeza, unaporuhusu Ufahamu kuingia kwako MUNGU anakusogelea ndio maana anasema wale wasio na Ufahamu wanakwenda kwa akili zao, walio na Ufahamu wanakwenda kwa Hekima na hapa ndipo Roho ya MUNGU anachukua nafasi kuwaongoza. Hata kiongozi wa Kiroho ni MZAZI wako kwa hiyo kama una Hekima UTAMUHESHIMU haijarishi yukoje, lakini wasio na Ufahamu watakwenda kwa akili zao na hapo zinawapa kutokuwa na Heshima. : Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments