ROHO WA HEKIMA

Tulipata kibali kupitia Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat E Mwingira kuomba roho tofauti za MUNGU,tushirikiane kuzifahamu hizo roho.Bwana Yesu atusaidie.

Roho ya Hekima inakupa: Inakupa kutenda na kusema mambo ya maana.

Efeso 5:15,16 (basi angallieni sana…. Mkiukomboa wakati) mtu anaepoteza muda ni Yule asiye na Hekima, ukiwa na Hekima inakusaidia kutumia muda vizuri maana muda hauongezeki bali unapungua maana siku hadi siku inakuruhusu Utajiri uingie kwako au umasikini uingie kwako.

Meth 16:1….(Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu bali jawabu la ulimi hutoka kwa MUNGU…) unavyoongea maneno yenye Hekima MUNGU anaingilia na kukusaidia, ukinena upumbavu MUNGU anayahukumu kwa hiyo angalia sana maneno unayoyanena, huwezi kunena vizuri kama huna Hekima, muda wote huu wa maombi MUNGU atakujibu sawasawa na ulivyo nena lakini ataangalia uliomba kwa Hekima?
Mfano:- Umeomba mume wako aokoke lakini ukienda nyumbani unafanya yasiyo na hekima kwa mume wako! Meth 16:9… kinywa cha mfalme kimejaa hekima. Ili uweze kufanikiwa hekima yako ndiyo inaongoza mafanikio yako. Jambo lolote inalomfanya MUNGU akukasirikie adui wa kwanza utakayekutana nae ni MUNGU mwenyewe, hata sasa hivi ukimuona mtu anafanikiwa katika biashara ujue Hekima ya MUNGU ipo pamoja nae, hata katika huduma yako omba Hekima, uwe Mchungaji, Askofu au viongozi wa cell ili kazi yako iende vizuri omba Hekima ya MUNGU sana, kwa sababu ukitaka kuongeza watu katika eneo lako lazima MUNGU akuongoze, ukitaka jambo lolote ili liende mbele zaidi Hekima ni ya muhimu. Unataka Kustawi Hekima ni ya muhimu kwa sababu dunia hii ina mitego mingi, kizazi cha uovu ni kingi sana hapa duniani bila MUNGU huwezi.

Chochote unachofanya kabla hujafikia maamuzi omba Hekima ya MUNGU hii itakuasa juu ya ubadae wako, hii ndiyo kazi ya Hekima kukupa mwangaza juu ya ubadae wako ni heri ukose hicho kizuri unachokiona kuliko kuharibikiwa ubadae wako. Hekima inakusaidia USIFIKIE mahali pa majuto, Hekima itakuondoa USIINGIE kwenye tatizo, linaweza kuwa jambo dogo tu lakini likamkwaza mwenzio na kufikia kuondoa Moyo wake kwako moja kwa moja, wakati wowote Hekima ITAKUSAIDIA usifanye upumbavu, kama kuna sehemu unahitaji nguvu ya MUNGU unahitaji HEKIMA, hata MAPAMBANO yako na ibilisi lazima utembee na Hekima, Bibilia inasema shetani ni mjanja kuliko Walokole, usipotembea na Hekima atakushinda. Bibilia inasema ‘huifundisha mikono yangu kupigana’, wengi mnafanya vitu na badae vikawaumiza wenyewe. Hekima itakuondoa kunako mtego.

Kwa sababu kujenga kunahitaji muda sana lakini kubomoa ni muda mfupi sana.

Kazi ya Hekima kwenye maombi.
• Hekima itakuambia sema hivi na hivi utaeleweka, iwe bosi, mtoto, mume, mke unaweza hujui jambo lolote lakini Hekima itakupa neno au swali la kumuuliza na kila iitwapo leo Hekima itakufanya UWE Bora. Katia Bibilia tunamuona Esta alikuwa na Hekima lakini huyu binti alikuwa house girl, wakati mwingine watu wengi walioowa ma housegirl wana nyumba nzuri na amani zao, kwa sababu binti wa kazi siku zote huwa anajifunza kunyenyekea, sasa kwa vile wewe mama umejifunza kutoa order na mumeo. Kwa nini Esta alishinda vita? ilikuwa si rahisi kwa hiyo hata alipokwenda kwa mumewe alikwenda kama anakwenda kwa mume, ni kwa mfalme alipoambiwa sema shida alisema andae chakula na akamtaja aje na adui wake, wa binti wa kazi hawaelezi wanavyonyanyaswa na wa mama huwa anasema anapokuwa ametoka katika ile nyumba, huwa anajifunza kusema kwa wakati, sipendi muwanyanyase hao mabinti na vijana maana hawakutaka kuwa hivyo ni yamemkuta, walee kama watoto wako na MUNGU atakubariki, ndipo Ester akaongea kwa Hekima na kwa mfalme mwenye Hekima hatoi hukumu mapema mpaka anajua umefika wakati muafaka, usije ukatoa maamuzi ambayo yatakuja kukumaliza wewe mwenyewe. Wababa waliozaliwa kwenye familia ya kishenzi wana matatizo sio wawajibikaji, ukiona baba yeyote ambaye hawajibiki anatoka katika familia ya kishenzi, Mwanamme mshenzi hajui mahitaji ya familia, washenzi huwapa watu maumivu, ukiolewa na mshenzi huwa ni mwaribifu siku zote hajali maana ni mshenzi, Mwanamme wa namna hi unaweza kumsaidia kumleta kwa YESU aweze kubadilishwa kutoka katika ushenzi na kumleta katika familia ya Kifalme, hapa haijarishi amesoma mpaka wapi, Usomi hauondoi ushenzi bali NGUVU ya MUNGU. Hata wa mama wapo washenzi na ukioa mshenzi utateseka maana utaleta hela ndani yeye anahonga wengine nje, huyo ni mshenzi. Je unataka kutoka katika ushenzi? tafuta Hekima ya MUNGU. Jamii ya kishenzi yeye haoni tatizo kuishi ukweni, Hekima ya MUNGU itakupandisha daraja ndiyo maana akasema mtu wa kwenu akipungukiwa na Hekima AOMBE.

• Ili MUNGU aweze kukupa Baraka za fedha anaangalia umepokea Hekima yake? ataona unaweza anakupa.
: Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.
 

Comments