Mtoto mpotevu aliporudi, alijiuliza kwanini nile na nguruwe, alirudi kwa baba yake, baba yake alimpokea kwa furaha zaidi. Sisi ambao tumeitwa Wana wa Imani lazima tuwabebe watu wasio na Imani tuwapende na tufanye kazi ya kuwaombea. Jinsi tunavyoendelea KUOMBA katika mwezi huu wa Maombi ndivyo MUNGU anavyozidi kutuinua na kuona MKONO wake na Machungu ya Watoto YATAISHA, machungu ya Wazazi YATAISHA, machungu ya maisha magumu YATAISHA, maana kutakuwa na FURAHA YA KUFURAHISHA. Najua siku ile ikifika utamwambia Mtumishi wa MUNGU asante kwa KUNIOMBEA, asante kwa KUNIONYA, asante kwa KUNIBEBA, leo unaona kama NAKUKOSEA lakini ile siku ikifika utasema ASANTE kwa kuniombea. : Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments