MAOMBI YA JANA (tarehe 21 May 2014) OMBA HIVI. 1. i) Uweke Mkataba/Agano na YESU KRISTO BWANA wetu, kisitokee chochote cha kukutenganisha, lazima kieleweke vyoyote itakayo kuwa lazima uingie mbinguni. Mkatabaka/Agano lako liwe katika NGUVU TATU (katika Damu ya YESU KRISTO, NENO LA MUNGU na JINA LA YESU KRISTO) Nguvu ya UWEZESHO iwe katika Hizi NGUVU TATU. ii) Mkimbize shetani ukiwa pamoja na YESU KRISTO BWANA wetu mpaka shimoni kuzimu. 2. Nitashinda kila upinzani na kila pingamizi kwa sababu nina NGUVU YA MUNGU. ANGALIZO: Hakikisha Mwana wa MUNGU Mwana EFATHA unakuja Kanisani kuhudhuria Ibada za Mafundisho na Maombi yanayoendelea kila siku katika Makanisa yote Efatha Ministry ndani na nje ya Tanzania, hakikisha unapata Maombi toka kwa Cell leader wako au Askofu wako kama hukudhuria Ibadani.

Comments