MAFUNDISHO Kutoka katika Mwezi wetu wa Maombi na Kufunga: (Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, "MTEMBEO WA MUNGU kwa hao Aliowaridhia") ROHO SABA ZA MUNGU Ukitaka kuelewa kitabu hiki; • Uwe na SIKIO la kusikia ili uweze kuona makusudi ya MUNGU, MUNGU akishaona unasikia anakupa MACHO ya kuona. Ulifikia TOBA kwa sababu ulikuwa na sikio la kusikia, ukishasikia unapata ile Neema ya kuona kupitia kuona tunatiwa Ufahamu. Rumi 1:1…(kama walivyokataa kuwa na MUNGU, MUNGU aliwaacha) Bibilia inasema ‘sikio na macho vyote vinatoka kwa MUNGU’, hapa anamaanisha kwamba ili usikie au ili uone unahitaji msaada wa MUNGU ukisema MUNGU hajakusikia si kweli maana wewe una Neema ya kuokoka hilo tu linamaanisha unamsaada wa MUNGU. Kusikia na kuona kunakusaidia kufikia toba, unapoendelea kusikia kupitia mafundisho utafikia toba na toba inakupa kibali cha kumuona MUNGU na anaposema kusikia Neno lake na kuona matendo yake ndiyo maana Isaya aliona na kutubu akasema ‘ole wangu mimi maana ninakaa katikati ya watu wenye midomo michafu’. Tatizo sio shetani ni maneno ya midomo yetu. Rumi 10:10 (kwa Kinywa mtu hukiri hata kufikia WOKOVU) • Kusikia na Kuona kunakupa toba; MUNGU hana shida ya dhambi ulizofanya ni ngapi lakini je umeelewa kwamba UMEKOSEA? tusiwe na maneno mengi mara ‘kwa sababu mimi sijasoma’ tatizo sio kutosoma tatizo umeelewa unachotakiwa kufanya? • Muda huu wa kufunga na kuomba ukweli ni kwamba, lengo ni Kusikia na Kuona na kisha tufikie TOBA na Toba itupe Ufahamu. • Toba inakupa MOYO safi, ukishaafikia mahali pa Moyo safi unamkaribia MUNGU naye anakupa. 1Kor 2:9 (macho hayajawahi kuona….) kumbe kuna kila kitu MUNGU amekuandalia je kwa nini unakwama? Kinachotutesa ni dhambi, zipo dhambi za kuwaza, kunena na kutenda, Je wewe unanena nini au unatenda nini katika maisha yako? Ebu fanya hesabu katika mawazo yako katika siku moja je mawazo yako yanakubaliana na ahadi za MUNGU na kama hayakubaliani na maneno ya MUNGU hiyo ni dhambi au kufanya jambo ambalo halikubaliani na mawazo ya MUNGU ni dhambi. Mwanzo 6: (mwanadamu mawazo anayowaza siku zote ni mawazo mabaya) Mwambie MUNGU yale uliyoniandalia nisaidie kuyafikia unapokwenda Kanisani, jitahidi kuondoa mawazo yoyote mabaya kisha nenda Kanisani. Jifunze kuishi kwa toba unaweza usipige mtu au usiuwe mtu lakini moyoni umeshajipiga na umesha uwa kwa kumuwazia mabaya!.

Comments