AINA ZA NGUVU Zipo aina 3 kubwa za Nguvu 1. Nguvu ya MUNGU 2. Nguvu ya uovu 3. Nguvu ya asili Katika hizi ni Nguvu ya MUNGU tu ndiyo inaweza kumuwezeshta mtu kufanya mambo Makuu, jifunze kubaini nguvu ipi inatumika. Kuna Nguvu ya MUNGU na nguvu ya uovu huwezi kujua nguvu ya uovu mpaka uwe na Nguvu ya MUNGU, masikini hawezi kujua uzuri wa utajiri bila kujua Nguvu ya Utajiri. Naamini ninyi wanangu mmeshapata Nguvu ya MUNGU, huo ni ufunguo wa kuingia sasa tafuta kuijua zaidi. Nguvu ya uovu siku zote inafanya kazi ya uharibifu, Zab:92: 7,9. Kumbuka kuna kizazi cha uovu ambacho kinatumia uovu, na kizazi cha dunia ambacho kinatumia nguvu ya dunia pia kuna kizazi cha wana wa MUNGU ambao wanatumia Nguvu ya MUNGU, ukiwa katika kizazi cha MUNGU hakikisha unatumia hii Nguvu ya MUNGU. Haya ndiyo mambo ya msingi sana kuyafahamu acha kulialia. Nguvu ya asili hii tunayo lakini na yenyewe inatoka kwa MUNGU. Ukiwa na Nguvu ya MUNGU itakusaidia kumaliza matatizo yako, wewe mwenyewe huwezi, ukiangalia watu wengi tumetoka katika familia zilizochoka, taka Nguvu ya MUNGU. Ukiwa na Nguvu ya MUNGU unaweza kuamrisha chochote na kikakufuata. Nguvu ya MUNGU ni ya muhimu sana kwa sababu inakutoa mahali pa uchache na kukupeleka mahali pa utele. Ukiwa na Nguvu ya MUNGU umasikini usahau, hata wabaya wakikufuata wanapigwa na hiyo Nguvu au umasikini ukikufuata unapigwa, uwe mjanja katika kupata Nguvu ya MUNGU, Nguvu ya MUNGU haipo tu kwa ajiri ya kufukuza pepo. Maisha yangu mimi Josephat ni Ushuhuda tosha, nilikuwa na tshirt moja imeandikwa pepsi, suruari moja, nguo ya ndani moja. Bibilia inasema “wenye dhambi wanatutwa na kutweka kwa ajiri ya wenye Haki” Nguvu ya MUNGU unaweza kukusababisha utoke katika mateso na machungu yanayokutesa. Unachohitaji si pesa, si ada wala mtaji unahitaji Nguvu ya MUNGU. Nguvu ya MUNGU ndiyo itakayowekea msukumo kwa watu kukuletea zawadi. Nguvu ya MUNGU inakutoa kunako ujinga, matatizo na mateso. Huwezi kufanikiwa kwa porojo taka Nguvu ya MUNGU ikutoe kwa gharama yoyote. Ukitaka muujiza wa pesa jifunze kutoa kwa waliofanikiwa, unaweza kuitumia Nguvu ya MUNGU kuhamisha ufukara kabisa katika ukoo wako, Nguvu ya MUNGU ni kwa ajiri ya kukufanya uishi vizuri. Mithali 8:17 -21 (Nawapenda wale wanipendao…) Ahadi ya MUNGU kwa wale wampendao ni mali si mali tu na kujaza hazina kwenye mifuko yao. MUNGU hafurahi kuona watoto wake hata sasa wanatembea katika shida! Sema hivi; “MUNGU NIPE KUTAMBUA UMUHIMU WA KUWA NA NGUVU YAKO KATIKA MAISHA YA WOKOVU WANGU” Katika wafalme ambao walizidishiwa Nguvu ni mfalme Sulemani, wakati wa Daudi baba yake hakuna vita hata moja iliyomshinda Daudi kwa sababu ya Nguvu ya MUNGU. Amina. :Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments