TUACHE KUFANYA TABIA ZISIZO MPENDEZA MUNGU: Vivyo hivyo tabia mbaya malipo yake ni laana. Mfano, Wana wa Israel walimwasi BWANA kwa kukataa kushika tabia ambayo waliagizwa watembee nayo matokeo yake wakashambuliwa na kushindwa vita. Tunasoma; “Ikawa ulipothibitika ufalme wa Rehoboamu, naye amepata nguvu, aliiacha torati ya BWANA, na Israel wote pamoja naye. Ikawa katika mwaka wa tano wa mfalme Rehoboamu, akapanda Shishaki mfalme wa Misri juu ya Yerusalemu; kwa kuwa walikuwa wamemwasi BWANA; mwenye magari elfu na mia mbili, na wapanda farasi sitini elfu; na watu wasiohesabika waliotoka Misri pamoja naye; Walubi na Wasukii na Wakushi. Akaitwaa miji yenye maboma iliyokuwa ya Yuda akaja Yerusalemu.” II Nyakati 12:1-4 (b) Vyanzo vya Tabia Vyanzo vikuu vitatu vya tabia ya mtu ni; Tabia ya kuzaliwa; Tabia ya malezi na Tabia ya kujifunza.....:Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Itaendelea kesho, Usikose Mwana wa MUNGU, NEEMA YAKO HII)

Comments