DARASA/KONA YA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea pale lilipoishia wiki iliyopita... KIRI katika UFAHAMU WAKO). MUNGU Akamwambia Nabii amimine mafuta kwa Daudi; familia nzima na jamii yote ikajua huyu ndiye Mfalme. Baada ya sherehehe hawakumtambua tena; akarudi machungani; waliona kama MUNGU Amekosea kwa Daudi kupakwa mafuta. Wengi wetu tumepakwa Mafuta na BWANA kuwa Matajiri wakubwa, Wafanyibiashara wakubwa, Viongozi wakubwa lakini bado mmekaa chini, maana hakuna anayekutambua, lakini saa inakuja ya KUTAMBULIKA KWAKO, sema HALELUYA. Siku moja Daudi akatumwa na babaye awapelekee chakula ndugu zake wakiwa vitani; alipofika kule akakuta wamekumbwa na tatizo linalosumbua Taifa zima. Akajitokeza kupambana na Goliathi na akamshinda! Sasa utamshinda adui yako na Yule anayetesa familia yako na ukoo wako kwa jina la YESU. Sema HALELUYA.

Comments

  1. Thank Apostle for teaching us God bless you .. I need to now. The end of this story about David mtumish we Mungu haleluy.... thank one's against ...

    ReplyDelete

Post a Comment