DARASA/KONA YA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea lilipoishia jana... Fungua UFAHAMU Wako) Mfano. Mwaka 1992 BWANA alinionyesha maono jinsi nitakavyokuwa. Ndani yangu niliamini lakini macho yangu yalipotizama Mazingira niliyokuwa nayo wakati huo, akili inakataa kukubaliana. Nilipofungua Biblia na kusoma inaniambia mimi Nitafanikiwa, Nitakuwa Mkuu, n.k. Kabla sijafika mwisho wangu nikasema, Niko tayari kukutumikia; mwaka 1992 Usingetamani kunisikiliza wala kuniangalia Usoni. Lakini leo MUNGU AMETIMIZA yale Aliyoahidi, leo watu wanaulizana “NI YULE YULE?” Nakutamkia kwa Neno la KINABII, “Ni wewe ambaye MUNGU anaenda kukushangaza, siku nyingi umeangalia wengine na kuwashangaa, sasa yanaenda kutokea kwako” SEMA HALELUYA!!. Hebu uwe Yusufu sasa na utunze maono hata katika Utumwa. Kuna wengi wamepoteza maono yao kwenye vitu vya kupita na sasa wamesababisha laana lakini huu ndio wakati kutambua hilo tatizo, hiyo laana na ukishagundua tatizo TUNATAFUTA DAWA; kama ni DAMU YA YESU Tutaialika; kama ni NENO LA KRISTO Tutalituma; kama ni KUKUWEKEA MIKONO Utawekewa, lazima UTOKE maana ni wakati WAKO wa Kuinuliwa, SEMA HALELUYA.

Comments