DARASA/KONA YA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea lilipoishia jana...Ubarikiwe) ''Tambua kinachokukandamiza! Wahubiri wengine watasema Kwa kuwa imeandikwa, “Hulituma Neno liwaponye, sasa nawaletea Neno la MUNGU, Amesema tena YEYE mwenyewe alichukua madhaifu na masikitiko yetu yote, …” Kwa kupigwa kwake sisi tumepona kwa hiyo pokea uponyaji! Siyo mgonjwa wala hana pepo! Miradi yake haiendelei, au watoto wanafeli shuleni, au ana matatizo katika ndoa hivyo tafuta kwa nini hayo yametokea, tafuta kiini cha tatizo! Mfano. Kuna mtu mmoja aliona maisha yake yameharibika na anakaribia kufa; alikwenda hospitali nyingi lakini hakupona, mwishoe hata hospitali wakakataa kumpokea maana hakutibika. Akaomba sana kwa MUNGU, MUNGU Akamwambia “Siwezi kukuponya mpaka uende kwa Mtumishi wangu uliyemtukana”. Alipokuja kwangu maana alikuwa ametamka maneno magumu sana juu yangu, akatubu kwa machozi; nikasikia HURUMA YA BWANA ndani yangu nikatamka Neno “Laana yako na ikuondoke”! Alikuja kwangu akiwa ameshikiliwa hawezi kutembea, baada ya laana yake kuondoka akatembea mwenyewe na UHAI ukamrudia! Ni vizuri kuelewa kinachokutesa, kumbuka “Watu wengi wanaangamia kwa kukosa maarifa” lakini kinachosababisha wakose maarifa ni kwa sababu hawajatambua UKWELI wa tatizo lake. “Utagundua SIRI na hiyo SIRI ndiyo UKWELI wenyewe na huo UKWELI Utakuweka HURU”. Omba! BWANA YESU niingize kwenye chumba cha Uchunguzi (xray); ROHO MTAKATIFU nisogeze kwenye Uchunguzi sasa nipime ee MUNGU Wangu.''

Comments