DARASA/KONA YA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea lilipoishia jana... darasa ni zuri, JIFUNZE UPATE KUJUA NINI KINAKUSHIKIRIA, NINI KINAKUTESA Ili Uweze KUKISHINDA KATIKA MAISHA YAKO) ''Zaburi 107:17 “Wapumbavu kwa sababu ya ukosaji wao na kwa sababu ya maovu yao, hujitesa”. Yawezekana unapitia mateso au maumivu ambayo yametokana na maovu yaliyofanyika huko nyuma labda wazazi wako kukosea au wewe mwenyewe kutokutii mambo ambayo MUNGU Amekuagiza. Kwa sababu hiyo unateseka; asili ya makosa siyo shetani. Tuangalie kwa ukaribu watu hawa: - Daudi alipakwa Mafuta lakini alipita njia za kufuatilia mpaka alipofika mahali pa kutukuka. Yusufu naye alipakwa Mafuta na MUNGU na akatamkiwa kabisa atakuwa nani, lakini akapita mapito magumu kabla ya ndoto yake au maono yake kutimia. Jitahidi kufuatilia UKWELI ili uwekwe HURU; wapumbavu kwa sababu ya upumbavu wao hujitesa, Nafsi zao huchukia kila aina ya Chakula. Wameyakaribia malango ya kuzimu. Maanake kila unachokifanya kinakufa na wewe unaona maumivu ya kifo, lakini Biblia inasema, “Wakamlilia BWANA na dhiki zao, naye Akawaponya na tabu zao zote”'' (Itaendelea kesho, Usipitwe Mwana wa MUNGU, ndio muda wako huu wa KUWEKWA HURU).

Comments