DARASA/KONA YA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias MwingiraEFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea lilipoishia wiki iliyopita, WEKA UFAHAMU Na Uelewe...) Asili haibadiliki, labda unaweza ukasema BWANA YESU Ameshughulikia laana zote; lakini ni vema ukafahamu ni laana ipi YESU Alishughulikia na ipi amekuachia Ushughulikie nayo. Imeandikwa, “Naye alituokoa kunako laana ya Msalaba” maana alishughulikia laana ya torati! Tunapoangalia kiini cha tatizo, ndicho kitakusaidia kutoka mahali kwenda pengine, ndicho kitakachokupa CHANGAMKO la Moyo. Dunia utaiona kama ni sehemu ya shangwe! Tatizo siyo shetani bali ni ile laana iliyotupata kwa kutokutii kwetu. Shetani yeye anafuatilia tu nani amelaaniwa na kushughulika naye. Mfano. Polisi humkamata mwenye hatia na siyo kila mtu; hivyo kama huna kosa hawashughuliki na wewe ila mwenye hatia ndiye wana uwezo wa kumfuatilia na kumkamata! Kama shetani ana nguvu za kukufuatilia, maanake kuna tatizo tayari! Kama MUNGU Anasema, “Mimi nitakuwa adui wa adui zako”! Ina maana kuna mahali tunajiletea shida sisi wenyewe. “Nami nitaijua kweli nayo kweli itaniweka huru”. SEMA KWA SAUTI Iwe ni sehemu ya UKIRI wako.

Comments