CHAKULA CHA ROHONI

umb 29:29 “Mambo ya siri ni ya BWANA MUNGU wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu na watoto wetu milele, ili tufanye maneno yote ya sheria hii. Mambo ya siri ni ya BWANA, wana wa Israeli walipokuwa utumwani Misri walitumikishwa na kuteseka sana lakini walipokuwa njiani wakiongozwa na Musa, kwa shida ndogo walitamani kurudi Misri (walitamani mambo ya nyuma, maisha ya nyuma). Kama HUJAKOMBOLEWA unawaza mambo matatu tu, KULA, KUVAA na KULALA. Wezi wote wala rushwa, mafisadi wanaiba ili Wale, Wavae vizuri na kujenga Majumba ya kifahari ili Walale. Huyu bado hajakombolewa. :- Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira.

Comments