HALELUYA,MUNGU WETU NI MZURI

Haleluya,... MUNGU wetu ni Mzuri, YESU wetu ni Mzuri, Tuna kila sababu ya kumwambia MUNGU Aliye BABA Yetu ASANTE, Leo Jumapili ilikuwa ni Siku nzuri sana kwa Wana wa MUNGU, Kwani BWANA wetu YESU KRISTO kupitia ROHO MTAKATIFU kwa Watumishi wake waaminifu (kuanzia Dar es Salaam Mwenge mpaka vituo vyote) Alitupatia Chakula cha Kiroho kizuri sana, Tulilishwa vya Kutosha, YESU Anatupenda sana, ndio maana Alitupa chakula kizuri cha Kiroho ili Tutoke mahali tulipo na kwenda kwenye Utukufu, na kwenda kuwa Huru... Kwa kweli MUNGU Wetu MKUU ni Mzuri sana, Anatupenda Wanawe.


Wana wa MUNGU wakitoa SADAKA ZA SHUKRANI kwa yale yote Mema Makuu ambayo MUNGU Amewatendea kwa wiki nzima, pamoja na ZAKA na Ya kutangaza INJILI pamoja na MASHANGILIO mbele ya Madhabahu ya BWANA MUNGU WETU MKUU.


Kipindi cha SHUHUDA, Wana wa MUNGU walitoka mbele na Kushuhudia Mambo Makuu ambayo MUNGU WETU MKUU, MUNGU Wa EFATHA MINISTRY Aliwatendea katika Maisha yao, ATUKUZWE na KUINULIWA Aliye BWANA MUNGU wa miungu, YEYE Aliye MWANZO NA MWISHO, Haleluya.


Comments