MANENO YENYE HEKIMA NA UFAHAMU

(Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira).

NGUVU YA LAANA NA JINSI YA KUONDOKA KATIKA LAANA.

Laana ni halisi na siyo kitu cha kufikirika.

Laana huanza kuonekana katika kitabu cha Mwanzo 3. Laana ina nguvu na nguvu yake imesababisha watu wengi kuteseka, nguvu ya laana Haionekani kwa macho lakini huonekana katika Utendaji wake au Matokeo yake.

Laana ina uwezo wa kuruhusu au kuleta au kusababisha Uovu na Uharibifu Utokee. Neno LAANA ni kinyume cha neno BARAKA.

Mwanzo 3:16 “Hakika nitakuzidishia uchungu wako na kuzaa kwako, kwa utungu utazaa watoto na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala”. Kutawaliwa ni sehemu ya laana! Mwanamke kutawaliwa si hiari yake bali ni sehemu ya laana yake aliyopewa na ukikataa unaishia Kuachwa au kupewa talaka.

Laana ya kwanza inamshambulia mwanamke- Kwa Utungu atazaa watoto; ule uchungu hauishii pale akizaa bali hata mtoto anapoendelea kukua hata kuwa mtu mzima yule mama bado anaendelea kusikia utungu mtoto likimtokea jambo zito. Mfano, mtoto akiumia, mama yake anasikia kushtuka kama ndiyo amerudishwa tumboni kwa upya. Ni kwa sababu ya ile laana.

Tunaposhangaa na kuona jamii ya watu wengine wanakuja Afrika na Kututawala ni sehemu ya Laana. Unaweza ukafika mahali mali yako inaliwa na wengine.

(Fundisho hili litaendelea kesho, Msikose Wana wa MUNGU, Lazima Mtoke huko, MUWE HURU!)

Comments