SIKU YA NNE YA KUSANYIKO LA EFATHA 2013

 Haleluya, Asante BWANA, Asante YESU kwa MASHANGILIO BWANA Haleluya.



 Ni Shangwe na Furaha nyumbani kwa BABA Yetu Aliye MUNGU Wetu MKUU wa PEKEE.... Kibaha Precious Centre kwenye Kusanyiko la BWANA MUNGU Wetu 2013.






Mafundisho na Mahubiri toka Kusanyiko KUU la BWANA MUNGU Wetu Aliye HAI MKUU, MUNGU WA KWELI; Kibaha Precious Centre 2013.

Mtumishi wa MUNGU: ASKOFU KITONGA toka NAIROBI KENYA wa KANISA LA REDEEMER CHURCH.

SOMO: AMANI
Watu wengi wanakwenda kanisani lakini hawana safari ya kwenda mbinguni!!. Wengi mnateseka na wengine mnanunua madawa kwa sababu mnateseka, Kwa nini Paulo aliwaambia Watumishi FURAHINI katika BWANA? Je ni kweli Watakatifu WANAFURAHI? Kweli ni kwamba HAKUNA kwa sababu bado wanahitaji AMANI, ninataka unaposhangilia USHINDI wa Efatha ruhusu AMANI kwanza, Waebrania 12: 14. Mara nyingi ninapohubiri ujumbe wangu wa kwanza kwa maskini ni ‘AMANI’ nilikuwa nikihubiri katika Kanisa kubwa nyingi Korea MUNGU akasema na mimi juu ya AMANI, na ninapohubiri AMANI mambo mengi makubwa yalitokea, je unajua familia nyingi Duniani hawana AMANI? Nchi n.k.

Ibilisi amesababissaha kutokuwa na AMANI. Paulo analiambia kanisa la Ebrania watafute AMANI ya YESU KRISTO, alisema AMANI iwe kwenu. Unapokuwa na AMANI kwa vyovyote vile UTAKATIFU utakuijia, anaendelea pasipo hiyo hamuwezi KUMPENDEZA MUNGU.

Kwa nini nilifundisha dhambi ya kukosa UPENDO jana ni kwa sababu roho ya MAIGIZO roho ya Yuda Eskaliote imejaa Makanisani! Huko Mbinguni hatuendi kwa vyeo vyetu tunaenda kwa UTAKATIFU, ndiyo maana Anasema TAFUTENI AMANI, unajua ni kitu gani tunakikosa ? TUMEKOSA AMANI. Mahali ambapo hakuna AMANI jua kwamba na UTAKATIFU haupo, na Uangalie kwa uangalifu kwamba mtu yoyote ASIPUNGUKIWE Neema ya MUNGU, unapofika mahali Ukaikosa NEEMA YA AMANI kinachofuatia hapo ni Uchungu na huyo ndugu Uchungu anafanya kazi pamoja na ndugu Matatizo, wengi ni Wasikivu wazuri lakini HAWATENDI kama NENO linavyosema, ndipo YESU Anasema ‘’Heri wenye Moyo safi’’ . UTAKATIFU unaambatana na AMANI, ukiishi kwa AMANI Duniani UFALME WA MUNGU utaishi Milele na Milele, wakati fulanii nilikwenda Uganda kuhubiri huko na nikaenda mji moja huko uitwao Mwenge, nikawa na washirika 4 kwa Mwaka mzima, Sadaka wakati mwingine shs 20 nikamwambia MUNGU nataka kurudi Kenya nikasikia sauti ya MUNGU ikasema “ NIMELIPA GHARAMA” kwa ajili ya BARAKA ZAKO, wengine mnataka MBARIKIWE lakini hampo tayari kulipa Gharama!!, nikaamua kwenda Mlimani kuomba kwa muda wa siku 4, siku ya kwanza mbu walikuwa wengi sana, siku ya 2 mvua, siku ya 3 Simba akaunguruma, siku ya 4 ndipo nikasikia sauti ya MUNGU ikisema “TULIA kuanzia Leo utakwenda katika Mataifa mengi kutangaza UZURI WA BWANA na UFALME” nikashuka . Sasa nilipolipa gharama nikarudi palepale kwenye mti, Mwanzo nilipokuwa nikihubiri kule mwenge nilihubiri ujumbe huu, mwanzoni nilikuwa Nikihubiri hawakuja watu, lakini baada ya kulipa gharama nilikwenda kuhubiri watu wengi walifunga maduka yao na kuja na WAKAOKOKA, wengi zaidi siku ya pili wakaja, nilialikwa kwenye Kongamano mahali Fulani, walikuwa ni watu wa Dini, nilipofika pale nilianza kupiga piano, ROHO MTAKATIFU akashuka, watu walikuwa hawajawahi kunena kwa Lugha, lakini Siku hiyo wote walianza kunena kwa Lugha hata bila kuwekewa mikono na kuombewa, Mchungaji wa pale baada ya kuona hayo alinichukua na kuniambia toka nje, Mchungaji Yule akanichukua na kunitupa nje. Niliendelea na huduma, nayo ikazidi kujulikana na kukua na kutambulika huko Uganda nilipoanzia.

Chochote unachofanya uwe na tabia ya mtu ALIYEOKOKA Ukilichukua NENO la MUNGU kama lilivyo, wakati tulionao ni wakati wa kufikiria UTAKATIFU, YESU alisema Neno Mathayo 5:9 (Heri wapatanishi maana hao wataitwa wana MUNGU), tunawapatanishi wangapi hapa?, nilipokuwa Israeli nilisimama palepale YESU alipokuwa akiwahubiria watu, nililia sana, Wamebarikiwa wanaowapatanisha watu. Jana niliwaambia Luka 21:25 maneno aliyoyasema YESU, 90% yamekamilika.
Zab. 34:14 Kama una uovu wowote huwezi ukaenda mbinguni, ni nani Anaekujua? sio Mtume wala mtu yeyote ila ni MUNGU mwenyewe, Unajua nini kinakuzunguka katika maneno, katika mawasiliano yako,
Kama wewe ni mtu unayetoa amri tu nyumbani na hutaki AMANI nini maana ya NENO, fuatilia yaani tembea nayo mstari wa Zab 118: 5 Nalimtafuta BWANA nae alinijibu,…

MUNGU Ametupa uwezo wa kuchagua, una uwezo wa kujitawala, YESU alisema AMANI nawaachieni, wengine wenu hapa unatakiwa umeze panado kwajili ya kichwa, magonjwa mengi yanataka AMANI ili yasikusumbue, kile unachokiwaza kinaweza KUKUCHIMBIA kaburi lako au KIKAKUFUNGULIA Mbingu,
Wengi mkifika sehemu za chakula mnawasumbua watu leteni chakula, wengine mnachimba makaburi yenu wenyewe, unapokuwa una AMANI unaweza kula sahani moja tu, lakini ukiwa hakuna AMANI unakula ovyo ovyo, AMANI ni dawa, itakufungulia Uwezo, itakufanya watu Wakutegemee, kwa sababu wewe una AMANI. Mimi popote ninapokwenda ninatangaza AMANI na mialiko mingi katika nchi wananiambia mimi ni mtu wa AMANI kwa sababu napenda kuhubiri AMANI.

Warumi 14:17,19 Ufalme wa MUNGU siyo kula na kula, jumlisha AMANI na furaha katika ROHO MTAKATIFU, unasemaje umepokea ROHO MTAKATIFU lakini wewe siyo mtu wa haki na AMANI, kama Kanisa la leo tukiamua kuongelea AMANI

Zab.85:5 (Nitasikia BWANA Anasema nini…) hebu fuatisha MUNGU Anachokufundisha katika kusanyiko hili, NENO hili linaweza kukufungua asubuhi ya leo kwa kusikiliza na kuamua, Utafunguliwa. Wakati umewadia kwa watumishi, ni Kulishughulikia swala la AMANI. Kuanzia leo uwe ni mtu wa AMANI na utakuwa mshindi. Watu watakuja kwako ili kupata AMANI uliyo nayo. Nina jumbe tofauti ninapofika kwenye ujumbe wa AMANI .

Yoh.14:27,. Je unataka kuwa Milionea? AMANI iwe pamoja na Wewe, unataka mafanikio? AMANI iwe pamoja na wewe. Wachungaji mnataka kuona mtu akifunguliwa mkiwaombea? AMANI iwe pamoja na ninyi. Je mnajua siri ya EFATHA? Apostle ni mtu wa AMANI, nimeshakutana na watu wengi sana.
Hes. 12:3 unajua Musa alikuwa ni mtu wa tabia gani? alikuwa ni mtu wa UPOLE ndivyo mtumishi MWINGIRA ni mpole, siri ya EFATHA kufanikiwa ni kwa sababu Mwanzilishi wake ni MNYENYEKEVU na ni mtu wa kutaka AMANI sana.

Ninakupa AMANI, YESU Alisema siyo kama vile Dunia inavyowapa, TANGAZA AMANI POPOTE UNAPOKUWA.
 
 

Breaking News:'' Mtoto wa Pili leo amezaliwa katika Hospital yetu ya Mashangilio katika mji wa BWANA MUNGU Wetu MKUU Kibaha Precious Centre, Mtoto amezaliwa na Kg 4, mtoto amezaliwa saa kumi na moja alfajiri, jina lake ni Sophia Wambura"

Asante YESU BWANA, Tunamshukuru MUNGU Wetu BABA MKUU kwa Matendo yake Makuu yanayoendelea Kwetu Wana Efatha, Asante YESU BWANA.

Comments