NYUMBANI MWA BWANA

 Tunamuabudu BWANA wa mabwana, MFALME wa wafalme,... YEYE ALIYEMUWEZA WAYOTE.
 " NENO, MAFUNDISHO, MAHUBIRI YA JUMAPILI Tarehe 27/October/2013 toka MADHABAHU YA KITUME na KINABII Mwenge Dar Es Salaam, EFATHA MINISTRY." - Mtumishi wa MUNGU Mama Eliakunda Josephat Elias Mwingira.

“MOYO WANGU UMEJAA SHUKRANI”
- Jifunze KUSHUKURU, utapata kuweza kuona mambo mapya katika maisha yako.
Isaya 12:1-6 “Na katika siku hiyo utasema, Ee BWANA, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeuka mbali, Nawe unanifariji moyo. Tazama, MUNGU ndiye wokovu wangu, Nitatumaini wala sitaogopa: Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Basi kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu. Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni BWANA, liitieni Jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa. Litajeni jina lake kuwa limetukuka……..”

Unaposhikilia jambo lako katika Ulimwengu wa roho, LITATOKEA. Unatakiwa UAMINI kwa NGUVU, Vita vyetu ni katika Ulimwengu wa roho, shetani hana jipya, ana COPY tu, ORIGINAL ilishachanwa, Copy amebaki nayo ili aone jinsi UNAVYOSHINDA.

Mpe YESU moyo wako, Anza KUFURAHI na YESU.

Kuanzia leo ebu anza KUJIFUNZA kutamka NENO Unalolitaka, anza KUSHUKURU, anza Kujifunza KUSHUKURU.

Anza KUJITAMKIA MAZURI, Unapotamka MAZURI yatasogea.

Unataka mke Mzuri; TAMKA Mke mzuri, Unataka Mume Mzuri; TAMKA Mume mzuri, Unataka Mtoto mzuri; TAMKA Mtoto mzuri, Unataka Jambo Zuri; TAMKA Jambo zuri, TAMKA VIZURI sasa.

Tangaza MAKUU ambayo MUNGU AMEKUTENDEA, Ukiyatangaza YANASOGEA.

Zaburi 37: 1-11 “Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya, Usiwahusudu wafanyao ubatili. Maana kama majani watakatika mara, kama miche mibichi watanyauka. Umtumaini BWANA ukatende mema,………….”

Angalia kile ambacho MUNGU AMEKUAHIDIA wewe, USIWAANGALIE wale watenda mabaya wafanikiwavyo, maana hao moto wameandaliwa tayari, hao ni wa moto tu.

Wewe ndiwe FURAHA ya MUNGU, MUNGU Alikuumba kwa mfano wake ili Afurahi, KINACHOMUUDHI MUNGU ni DHAMBI.

MUNGU Wetu Anatuwazia mema, Mawazo yake ni ya AMANI Kwetu.

Ushamwambia BWANA haja ya MOYO, sasa Mpe NAFASI Afanye.

BEBA Sifa za BWANA ndani ya Moyo WAKO.

Iko RAHA katika Kumtegemea BWANA, Ipo FURAHA katika KUMTEGEMEA BWANA.

Zaburi 37:1-11

- Utatafuta ugonjwa wako, hutauona tena, wale waliokuwa wanakushambulia hutawaona tena, Tatizo lako hutaliona tena.
- Toa MATAKATAKA yote ndani ya Moyo wako, Toa UCHUNGU wote ndani ya Moyo wako, maana huo MOYO utapelekea mwili wako kwenye MAANGAMIZI.
- Moyo wako UTAKAA na BWANA, Umeamua KUTEMBEA na BWANA.
- Kaa na BWANA, ili UFURAHIE VYA KIFALME.

BWANA Anawacheka maadui zako, maana YEYE ndiye Mpiganaji vita.

Ukipata AMANI, Umepata AFYA Njema, Unapokosa AMANI Unakuwaje?. Tafuta AMANI ya KRISTO, kuna watu wanafanya maamuzi mabaya kwa sababu WAMEKOSA Amani, walikuwa wana hasira.

Hasira HASARA, Wewe kwa Mtu Uliyeokoka usiwe na Hasira, Ukiwa na Hasira MWITE BWANA YESU Akupe AMANI.

Usikubali KUSHINDWA, Taka MASHAURI YA ROHO MTAKATIFU, Mwenye Hekima ya MUNGU hafanyi mambo kwa Hasira.

ANZA Mazoezi ya KUSHANGILIA, Anza mazoezi ya KUMTUKUZA BWANA.

KITU MUHIMU: LINDA MOYO WAKO, Maana Moyo wako Ukiwa na Amani UTAPATA YOTE.

Mpe Moyo wako YESU, SI Binadamu, Binadamu Watu WATAUTOBOATOBOA.

Unamuweka MTU Moyoni, UNAMBEBA Mtu Mwenye Kilo kama 85 MOYONI, huoni Unajiangamiza?

FURAHA YAKO si MUME, Si WATOTO, si MKE, si NYUMBA NZURI,…. BALI NI YESU. Maana Watoto Wataolewa au Wataoa, Mume anaweza kuwa Safari au kuwa MBALI nawe, LAKINI YESU HAWEZI Kukuacha.

MUNGU HATAKI Kuona KITU Kinaingilia kati yako na YEYE, kama Mume ndio Anakufanya uwe mbali na YEYE MUNGU, unaweza kushangaa Mume wako ANAONDOLEWA, Kitu CHOCHOTE kile KISICHUKUE nafasi ya MUNGU.

Kuna watu ndoa zao ZIMEKUFA kwa sababu Waume zao walichukua Nafasi YA MUNGU.

Na MUNGU NI MWENYE WIVU Sana (Imeandikwa: MIMI NI MUNGU MWENYE WIVU), Akiona UNAMSAHAU kwa sababu ya KAZI, au BIASHARA, au MUME, au MKE, au WATOTO, au SHAMBA, N.K, MUNGU ANAWEZA Kuviondoa hivyo vyote ili AWE KARIBU NA WEWE.

WOKOVU ni Nuru, ni Taa; kwa hiyo Watu WAIFUATE TU.
Zaburi 119: 105
Zaburi 119: 36

Ukiwa na BWANA (WOKOVU) Utapata AKILI NZURI na KIBALI.
Mithali 6: 16-18 “Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;


Comments