SOMO: "NGUVU YA MUNGU"
Roho Mtakatifu anapokuja, anabeba Upendo wa Mungu, Neema na Nguvu ya Mungu. Kwa hiyo Roho Mtakatifu anapokuja kwa mtu, yupo pale ili kuwakilisha mambo haya matano ambayo ni; UPENDO, NEEMA, UTUKUFU, NGUVU na UPAKO. Kwa hiyo mambo haya matano yapo pale ili kumkamilisha Mwamini.
Ni MATAMANIO na MAPENZI ya Mungu wanawe wajawe na NGUVU ya MUNGU. Unahitaji Nguvu kwa sababu ibilisi naye ana nguvu. Na ni yeye anayetawala dunia na anawafanya watu wawe maskini, wafanye dhambi, wateseke n.k…
- Unahitaji Nguvu ya Mungu ili uwe juu ya Nguvu za giza. Kama huna Nguvu na umeoa au kuolewa, mapepo yatashambulia ndoa yako. Nguvu ipo pale ili kukuwezesha kuyashinda mazingira yako.
Matendo 1:8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”
Nguvu ni kama gari linalokubeba na kukupeleka kazini, pia ni kama CHOMBO kinachokuwezesha kufanya Kazi. Unajazwa na Nguvu pale Roho wa BWANA anapokuwa juu yako. Roho Mtakatifu ndani yetu ndiye anayetufanya kuwa Wana wa Mungu.
- Roho wa BWANA juu yako ndiye anayekusaidia uwe na Nguvu ya Kuujenga Ufalme wa Mungu.
Roho wa UWEZA ndiye anayebeba Nguvu na kuiachilia ndani yetu ili kutuwezesha kuikamilisha KAZI ya Mungu. (Roho wa UWEZA ni kwa ajili ya UFALME). Hayupo pale ili kukuwezesha wewe ule bali yupo pale ili kukuwezesha ujenge UFALME wa Mungu mfano kupitia kufanya Biashara n.k…
Waefeso 3:20 “Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu”
Roho wa BWANA anapokuwa juu yako, anakuwezesha kuyaona Maajabu ya Mungu na kufanya Kazi kwa wepesi bila kuhangaika. NGUVU IPO PALE KUYAFANYA MAISHA YAKO KUWA MEPESI.
© Mtume na Nabii Josephat E. Mwingira (Efatha Ministry)


Comments