USHUHUDA:
Naitwa Miriamu Mosha kutoka Arusha :
Nilipata tatizo la kuumwa kichaa kwa muda wa miezi sita, nikawa nakula mende na funza na nilikuwa naishi kwa kunywa dawa na sindano.
Pia nilikuwa natumikishwa na nguvu za giza kwani nilikuwa naenda kuzimu .na huko nilikuwa napata mateso mengi. Ndugu zangu walikuwa wamekata tamaa kutokana na hali niliyokuwa nayo, siku moja dada mmoja akaongea na mume wangu kuhusu kuja katika Kusanyiko, akidai kuwa kuna uponyaji. Mume wangu alikubali na kunileta kwenye Kusanyiko .
Nilipofika katika kusanyiko lile wakati Ibada inaendelea mahali nilipokuwa nimekaa Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alimsogelea mtu mmoja akamuombea kwani alikuwa anateswa na roho za kichawi, na akasema wale wote walioteswa na nguvu za kichawi wanafunguliwa katika Jina la Yesu.
Alivyosema vile niliona kama ndani yangu napingwa shoti ya umeme, nikawa mmoja wa walio pokea uponyaji papo hapo.
Pia nilikuwa nasumbuliwa na ugonjwa sugu wa vidonda vya tumbo na macho, nimevaa miwani kwa muda wa miaka 20. Namshukuru sana Mungu kwa kuniponya yote yaliyokuwa yananitesa, leo namtukuza Mungu, sina cha kumpa bali shukrani za moyo wangu.

Comments