USHUHUDA:
Naitwa Katherine Rogasiani. Namshukuru Mungu kwa kunifanya mtu mkuu kwani Yesu alinitoa chini na sasa ameniinua. Nilikuwa nafanya biashara ndogo ndogo nikawa na malengo ya kuwa mfanyabiashara mkubwa. Katika hiyo biashara niliyokuwa nafanya nilifanikiwa kufungua Akaunti ambayo ilifikia kuwa na kiasi cha shilingi milioni moja na laki nane.
Wakati huo nilikuja katika kusanyiko Kuu hapa Efatha Ministry Precious Center, Baba Mtume na Nabii akatangaza kuwa ‘watoto wangu nataka mshiriki Baraka za kuwarudisha wageni waliokuja kwenye Kusanyiko. Na mimi nikatoka ili kumtolea Bwana japo moyo wangu ulikuwa unauma na kukataa. Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alivyozidi kusisitiza, nilitoka mbele na kutoa kile kiasi chote kilichokuwepo kwenye Acount yangu.
Nilimshangaa Mungu kwa matendo yake makuu kwani baada ya kumtolea Mungu alinibariki. Nimejenga nyumba nzuri na ya kupendeza. Namshukuru Mungu ameniinua kwa kiwango cha juu. Nawashauri wana wa Mungu, tuwe watii kwa Neno linalotoka kinywani mwa Mtumishi wa Mungu maana katika Kutii ndiko kuna baraka zetu .

Comments