USHUHUDA:

Glory Saidy, Namshukuru Mungu kwa kuniponya kwani nilikuwa naumwa ugonjwa wa kupooza kwa muda wa miaka mitatu. Kwa muda wote huo sikuweza kufanya chochote kile, nilikuwa siwezi kula mwenyewe mpaka nilishwe, siwezi kuvaa nguo wenyewe na hata kuoga.

Nilipoletwa hapa kwenye Kusanyiko la mwaka jana 2016 Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alisema wagonjwa wote waliokuja watarudi wakiwa wamepona, nililipokea lile Neno na baada ya maombezi nilipokea uponyaji wangu. Namshukuru sana Mungu kwa kuniponya kwani nilikuwa siwezi kufanya kazi yoyote, lakini sasa naweza kufanya kazi zangu zote

Comments