SOMO: NGUVU ZA MUNGU:
Kuna aina tatu za Roho :
• Roho Pamoja nasi: Roho huyu anatusaidia sisi kujihukumu na tuweze kutubu ili kwamba tuweze kumpokea Bwana Yesu.
• Roho ndani yetu;Roho huyu ndiye anayetuwezesha sisi kuwa wana wa Mungu na ndiye anayeitwa Roho wa Kristo. Pia anakusaidia kunena kwa lugha na kukataa dhambi
• Roho wa Mungu juu yetu; Roho huyu anatuwezesha kuwa na Nguvu ya Mungu, ili kwamba tuweze kuujenga Ufalme wa Mungu. Na ndiye anaitwa Roho wa Uweza, na ndiye tunaye muita Nguvu.
Roho ya uweza ndiyo inayobeba Nguvu ili kutuwezesha kufanya kazi ya Bwana.
Roho ya Upendo na Neema ni kwa ajili yako, lakini Roho ya Nguvu ya Mungu ni kwa ajili ya Ufalme na haiko ili kukusababisha wewe ule au uvae nguo nzuri la ! bali ipo ili kukuwezesha wewe kufanya kazi kwa ajili ya Ufalme wa Mungu.
Waefeso 3:20 “Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;”
Roho ya Mungu inapokuwa juu yako inakuwezesha wewe kupokea maajabu ya Mungu katika maisha yako, hii inakusaidia wewe kufanya kazi kwa wepesi bila maumivu. Nguvu iko ili kukusababisha maisha yako kuwa mepesi. Katika uwepo wa Nguvu ya Mungu kuna kuwezeshwa, kuna mtembeo wa udhihirisho wa Roho Mtakatifu

Comments