ROHO YA KUMCHA BWANA:
Palipo na Neema ndipo palipo na Shukrani, kwa sababu Neema ndiyo inayo kusaidia wewe kuwa na moyo wa shukrani. Ukiwa na Roho wa kumcha Bwana usifanye yasiyo mpendeza Mungu maana Roho hii inaweza kukuua.
Kwa nini asilimia kubwa ya watu wanakuja Kanisani na kuomba sana lakini bado wako vile vile? Kwa sababu Neema ya Mungu haipo kwao.
Neema ndiyo inayoleta mabadiliko kwa mtu. Mfano:- Mtu akiwa na mabadiliko yoyote yale au kitu kizuri kinapo tokea kwake hata watu wengine wakimwangali wanasema kuwa, mtu huyo ana Neema. Ni Neema tu ndiyo inayoweza kumfanya mtu abadilike, bila Neema hakuna mabadiliko yoyote yanayoweza kutokea kwa mtu.

Comments