MTUMISHI WA MUNGU GARY WINSTON:
MUNGU ANATARAJIA NINI KWAKO, NA MIMI KAZI YANGU NI NINI?
Waebrania 10:19 “Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, ” Mungu anakutarajia wewe uweke kidole kwa adui zako na kuwafukuza, kwa sababu Yesu alikwisha kulipia hayo yote, adui yako hana mamlaka juu yako, unacho takiwa ni wewe kuelewa tu kuwa wewe ndiyo una mamlaka juu yao. Usijiwazie vibaya kuwa bado unadhambi bali amini kuwa umesamehewa.
Mtu yeyote anayejaribu kujilipia dhambi zake inamaana kuwa ni sawa na anamwambia Yesu kuwa hakufanya kwa ukamilifu pale msalabani.
Kama huna ujasiri na Mungu kamwe hutakuwa na ujasiri na ibilisi huku duniani, atakutesa tu, jiamini kuwa wewe ni mwana wa Mungu na uwe na Ujasiri na Baba yako.
Bwana Yesu alipokufa pale Msalabani, Je! Furaha yake ilikuwa ni nini? Furaha yake ilikuwa ni kutimiza mapenzi ya Baba yake, Baba yetu wa Mbinguni anatupenda sisi kwa sababu sisi ni furaha yake na ni changamko kwake.
Wagalatia 2:20 “Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. ”
Mungu anatarajia adui zako uwaweke chini ya miguu yako.
Mungu amekuita ili usimame, usipo simama adui zako hawapo chini ya miguu yako.

Comments