KUSANYIKO KUU LA TISA PRECIOUS CENTER KIBAHA.
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA:
SOMO: NGUVU YA MUNGU:
Roho anapokuja amebeba Upendo, Neema na Nguvu za Mungu.
Roho anapokuja kwa mtu yupo ili kusababisha mambo matano:-
1. Upendo
2. Neema
3. Nguvu
4. Utukufu na
5. Upako
Mambo hayo yako ili kumkamilisha mwamini ili awe tayari kwa ajili ya Kristo na awe tayari kutumiwa na Mungu. Huwezi kumtumikia Mungu mpaka akazidisha Upendo wake kwako bila Nguvu zake.

Roho anapokuja kwako anakuja na Roho saba za Mungu kama Mkono wa Mungu, hivyo wanapo kuja wana dhihirisha upendo, nguvu, utukufu na Upako.
Bila kuwa na Roho ya Hekima na Ufahamu, huwezi kumpenda mtu usiye mjua hivyo unahitaji kumfahamu mtu huyo kwa sababu huwezi kuwa katika mahusiano na mtu usiye mpenda kwa sababu unaweza kumuumiza. Hekima inakusaidia kupenda kwa busara kwa yule umpendaye. Upendo unapokuja kwa mtu unakuja na Roho hizo mbili.

Comments