KUSANYIKO KUU LA TISA
PRECIOUS CENTER KIBAHA SIKU YA TANO.
ASKOFU: CHARLES KARIUKI KUTOKA KENYA
Luka 19:9 “Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu. Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. ” Ni watu wangapi walikuwa pale alipokuwa Zakayo? Walikuwa wengi lakini Yesu alimuona Zakayo tu.
Kwa nini Zakayo peke yake?

• Zakayo alikuwa ni tajiri. Luka 19:1-2 “Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake. Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri. ”
-.Zakayo alikuwa na shauku kwa kile ambacho alikuwa anataka kukiona (yaani alikuwa anataka kumuona Yesu). Unapaswa kuwa na shauku ili uweze kumuona Yesu katika maisha yako.
• Zakayo alikuwa mmoja wa watoza ushuru , huyo ni mwana taaluma na ni mtu aliyesoma na kuinuliwa katika nafasi yake ya kazi.
Mungu hakuumba watu wafupi wala warefu bali aliumba watu wa thamani kwa sura na mfano wake.
Kila mmoja wetu aliumbwa tajiri, kwa sababu vinasaba vyetu vinatokana na Mungu aliye Baba yetu ambaye yeye ni tajiri, sisi ni matajiri kwa sababu ya uumbaji.
Sisi tunaonekana ni maskini kwa sababu ya wale majirani zetu ambao wanaendesha magari lakini kama wakiwa hawapo sisi ni matajiri.
Hata Zakayo hakuwa mfupi bali kwa sababu ya wale ambao aliokuwa nao ndio walimfanya onekane kuwa ni mfupi.
Sababu inayokufanya wewe ujiite kuwa ni maskini ni kwa sababu unajilinganisha wewe na watu wengine. Usijilinganishe na mtu mwingine kwa sababu Mungu alikuumba wewe kwa namna ya kipekee haufanani na mtu mwingine.

Comments