ASKOFU JOSEPH KAZHILA
SOMO: IMANI.
Habakuki 2:10 “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. ” Mwenye haki ni nani? Ni mwamini, yule ambaye amekubaliana na Neno la Mungu.
Warumi 1:16 “Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. ” Injili ni Nguvu ya Mungu iletayo Wokovu.
Mungu aliupenda sana Ulimwengu na ndio maana alimtoa mwanawe wa pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.
Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.” Kama huwezi kuamini utaaibishwa, Wakristo wengi wameaibishwa kwa maradhi, magonjwa na umaskini kwa sababu hawamwamini Mungu.
Mungu anatafuta watu wadhaifu ili kuwafanya kuwa majasiri kwa ajili ya kazi yake na ili Utukufu umrudie Yeye.

Comments