ASKOFU JOSEPH KAZHILA
SOMO: IMANI.
Kuna Wakristo wengi wana amini kwamba ukisha kuwa na IMANI hawahitaji kwenda Hospitali, mimi ninaweza kusema kuwa hiyo si IMANI ya kweli kwa sababu Madaktari waliopo Hospitali wamepata akili ya kufanya hivyo kwa Mungu mwenyewe, IMANI haikiuki mamlaka bali inaheshimu mamlaka.
Waebrania 11:1 “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. ”Imani ni nini? Imani maana yake ni kua na kitu unachokitarajia hivyo unapaswa kuwa na uhakika wa kile unachokitarajia kuwa kitakuwa, ili kiweze kutokea.
Imani ni kitu kinacho wezesha tumaini kutokea.
Warumi 10:17 “Basi Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. ”
Imani inakuja kwa kusikia hivyo utakapo sikia Neno la Mungu unaweza kuwa na Imani. Kamwe hutaweza kuwa na Imani nje ya Neno la Mungu.

Comments