ASKOFU CHARLES KARIUKI KUTOKA KENYA:
SOMO: WEWE NI NANI NA MUNGU AMEWEKA NINI NDANI YAKO.
Mwanzo 1: 26 -28 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba……”
Tatizo kubwa tulilonalo huku Duniani, ni watu kutokujitambua. Kama hujitambui huwezi kujua una nini au uwezo wako wa kutenda ni upi. Kuna baadhi ya watu wana amini kile ambacho ma-babu zao waliwaambia, na wengine wana amini kile ambacho waalimu wao Waliwaambia, na kwa sababu waliwaambia madhaifu mengi sana kuhusu wao na hivyo ndivyo wanavyojichukulia.
Mungu alipo mtokea Gideoni na kumwambia wewe ni mtu shujaa, Mungu alijua kuwa Gideoni ni shujaa lakini Gideoni mwenyewe alikuwa anajiona tofauti. Gideoni alijiona dhaifu kwani alikuwa anajificha mbele ya jeshi la Wamidiani. Gideoni aka anza kujielezea kuwa familia yake ilikuwa ni maskini na yeye pia alikuwa maskini hivyo akakataa kuambiwa kuwa ni shujaa.
Mungu kamwe habadilishi kile ambacho alikinena, na hayuko tayari kubadilisha kile ambacho amekinena. Unapaswa kubadilisha akili yako, kwa sababu Mungu habadiliki kamwe. Kile ambacho MUNGU anakijua kuhusu wewe ni kweli, tofauti na kile ambacho unakijua kuhusu wewe ambacho maranyingi e ni uongo.
Mungu alimwambia Gideoni kuwa ana nguvu ya kuokoa taifa na si familia yake tu. Pale alipokuwa anajificha si mahali pake, yeye ni mkuu hivyo achukue nafasi yake ili afikie ukuu wake.

Comments