PASTOR MICHAEL OLAWARE KUTOKA UK (KATIKA KUSANYIKO KUU 2016) SOMO : KUVUNJA KIZUIZI MBELE YAKO Isaya 54:1-4 “Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema Bwana. Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako.” Mungu anataka uimbe na ushangilie, wewe ni wamuhimu sana mbele za Mungu Mungu hafurahii kukuona unahuzuni bali anafurahia kukuona ukifurahi, wiki hii utaimba wimbo wa Bwana. Imba wewe uliye masikini wewe uliye tasa imba kwa maana kutakuwa na upenyo na mabadiliko yanakujilia. Panua imani yako ongeza uzao wako maana Mungu anafanya jambo jipya kwako.


Comments