KUSANYIKO KUU 2016 LIVE (KUTOKA PRECIOUS CENTER KIBAHA) NENO UUMBAJI WA MUNGU - MCHUNGAJI DAVID MWAKISOLE (Mwanzo 1:1,26-27 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.) Mungu ndiye aliyeumba Mbingu na nchi naye ni Mungu aliye hai, Yeye siyo Mti Jiwe wala Mlima bali ni Mungu aliye hai. Mahali popote utembeapo ukaona Mlima mkubwa Mti mzuri au chochote ukionacho ujue aliyekiumba ni Mungu. Mungu alimuumba mtu kwa sura na mfano wake hivyo wewe ni sura na mfano wa Mungu ni kazi ya Mungu, wewe hujatokana na kiumbe chochote, mwanadamu hajatokana na nyani, shetani aliweka akili hii kwa wanadamu ili wajue kuwa wametokana na mnyama kwa sababu alijua kuwa mwanadamu akijua kuwa amefanana na Mungu hatampata hata mmoja. Mungu ni Roho hivyo na wewe ni Roho Mungu alisema nendeni mkatawale hivyo wewe ni mtawala dunia pamoja na Mungu. Dhambi ikiwepo kwako inakunyima kutawala na kumiliki hivyo achana na dhambi urudi kwenye heshima yako ambayo Mungu amekuwekea, Ili Mungu akufurahie anza kutenda mapenzi yake.


Comments