Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira:
Unachochea kipawa chako kwa kufanya kazi ya MUNGU kwa bidii, ukisikia kusaidia watu saidia bila kunungunika. Acha MUNNGU atumie MUDA wako na MALI zako.
-Kipawa kinakutoa katika watu wadogo na kukuketisha na watu wakuu. Ukipata kipawa unahamishwa kutoka daraja la chini na kupelekwa daraja la juu. Kipawa cha Mungu kinakupa kumwambia MUNGU nafasi yako ni hii, na yeye anakutoa daraja la chini na kukupeleka daraja la juu. Kipawa kikimvaa mtu kinampa kubainisha tabia hii HAPANA, utapeli hapana na wizi hapana. Kipawa lazima kikupe kushinda ukiona unashindwa ujue kunamahali umetelekeza kipawa chako.

Comments