SOMO: NGUVU YA UWEPO WA MUNGU MCHUNGAJI MICHAEL OLAWARE Ili uweze kusonga mbele unahitaji uwepo wa Mungu Kutoka 33:12 "Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako." Musa alikuwa mtu mwenye busara, Musa alikuwa na hekima na wewe ukajifunze kutoka kwa Musa, Musa akamwambia Mungu nionyeshe njia si vile ninavyotaka mimi bali vile unavyotaka wewe. Huduma ya Efatha Mungu anakwenda kutupeleka mbele na kutufanya watu wakuu na anavyotupeleka mbele atafanya njia yake. Maombi yako siku zote omba Mungu akuonyeshe njia yako. Penye uwepo wa Mungu panakuwa na mahusiano kati ya mtu na Mungu. Ukiwa na uwepo wa Mungu unakuwa na Roho saba za Mungu, zitakazo kupa mafanikio katika maisha yako. 1wakorinto 9:24"Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate." Kila unachokifanya katika maisha hakikisha unakifanya ili kufanikiwa, iwe ni kwenye ndoa, biashara, huduma, usifanye ili kushindwa bali fanya ili uweze kushinda. Jifunze kujidhibiti mwili wako kwasababu mwili wako ni wathamani na ni hekalu la Roho Mtakatifu usiweke madawa ya kulevya, pombe kwenye mwili wako pia jifunze kutembea kwenye kusudi, Kutembea kwenye mapenzi ya Mungu , kila kitu kinakusudi hapa chini ya jua lazima ujue kusudi lako uwe na malengo na ujijue kwa nini upo hapa, kwa nini upo Efatha, usiishi maisha ya mwingine. Mungu ni mwenye makusudi dumu kwenye makusudi yake. Kwenye biashara zako unahitaji njia ya Bwana. Haijalishi umefankiwa kiasi gani unahitaji uwepo wa Mungu, usithubutu kufanya kitu chochote nje ya uwepo wa Mungu. Zaburi 114:1-5 "Haleluya. Israeli alipotoka Misri, Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni. Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake. Bahari iliona ikakimbia, Yordani ilirudishwa nyuma. Milima iliruka kama kondoo waume, Vilima kama wana-kondoo. Ee bahari, una nini, ukimbie? Yordani, urudi nyuma?" Kama bahari ilivyo kimbia na wana wa Israel wakapita vivyo hivyo kila mazingira magumu yatakavyo kimbia katika maisha yako. Kila kizuizi kitapisha njia chenyewe kwasababu umebeba uwepo wa Bwana na nguvu za shetani ziitaachia. BARAKA ZA UWEPO WA BWANA • Ukiwa na uwepo wa Bwana unapewa pumziko, • Ukiwa na uwepo wa Bwana unapata kibali, • Ukiwa na uwepo wa Bwana unapata ushindi, • Uwepo wa Mungu utakupa ulinzi , • Uwepo wa Mungu unakupa uongozi na mwelekeo • Uwepo wa Bwana unakupa mahitaji. • Ukiwa na uwepo wa Bwana Mungu atakupa afya VITU VITATU VILIVYOSABABISHA MUSA AFURAHIE UWEPO WA BWANA 1. Aliweka usikivu wake wote kwa Mungu ,Mungu anapokuita anataka uwe naye tu, hataki uwe na mengine. Kutoka 3:2 "Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.." 2. Musa alitoa kila alichonacho kwa Mungu kutoka 4:19 "Bwana akamwambia Musa huko Midiani, Haya, nenda, karudi Misri; kwa kuwa wale watu wote waliokutaka uhai wako wamekwisha kufa." 3. Musa alikuwa ana tegemewa na alikuwa msikizi, unahitaji kutegemewa na unahuitaji kuwa na uwepo wa Bwana ili uweze kuingia katika nchi ya ahadi.

Pichani; Mtumishi wa Mungu Mchungaji Michael Olaware kutoka Uingereza akitoa Neno la Mungu katika Kusanyiko kuu ndani ya mji wa Bwana Precious center Kibaha. Jinsi upendo wa Mungu usivyokuwa na ukomo kwa Mwanadam. Hupaswi kukata tamaa, wala kukwazika kisa umetengwa, wala kujihisi upweke na kujiona mwenye dhambi sana ikakufanya kushindwa kumwabudu Yeye. Mungu wetu upendo wake ni endelevu, mwendee kwa maombi huku ukiuachilia Moyo wako kwake maana upendo wake hauna kipimo naye atahuisha nafsi yako

SHUHUDA:Naitwa Ester Emmanuel: Napenda kushukuru Mungu kupitia mchungaji Michael kutoka njee ya nchi, alihubiri akasema kuna mtu anaitwa Ester ana neno aliambiwa na Mungu na asipolifanyia kazi litageuka na kumfanya awe kinyago, nanilimuona Raisi Nyerere akiididimiza chini kuzimu na mimi nikaamrishwa kutamka maneno nikaamuru na pia nikawa nina kutana na Raisi Mwinyi nayeye pia hivyo hivyo na pia nikamkuta pia anadidimiza nchi na mwishowa siku nikamkuta mtu mwishoni akanyanyua ngumi kwa ushuhujaa mkubwa natukawa tumeshinda

10 things to help you thrive:- 1. Be connected to God. John15. Without God you cannot do anything. For a man to prosper he has to be connected to His source of power. 2. Become planted in the house of God. Those planted in the house of the Lord will flourish. To get profit off the Lords house, you must be planted in the house of the Lord. “Be rooted”. 3. Expose yourself to the right environment. Be careful where you expose yourself. If you have a friend who does not add value to your life, leave him/ her and move on. 4. Discover your true worth. Nobody will tell you what you are worth. The only person with the right to tell what you’re worth is your manufacturer. The word of God is your manual. 5. Nurture your heart and order your words. You must protect your heart. If there is anything that you need to protect more than anything; it’s your heart. 6. Put your light on a candlestick. Isaiah 60 (Arise and shine) Let your life shine 7. Unleash your potential. Everybody has something to offer. God breathed in mans nostrils; and in that breath there is potential that is not discovered. You have the responsibility to stir up your potential. You have what it takes for your prosperity. You have something inside worth discovering. 8. Renew your mind Rom 12. 9. Be filled with the Holy Spirit Pastor Michael UK

NENO

August 21, 2015
Efeso 1:3 "Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Maana, katika kuungana na Kristo ametubariki kwa kutujalia zawadi zot...

IMANI

July 30, 2015
 UNAPOAMINI Yale YASIYOONEKANA Unathibitisha kwamba:- - MUNGU ni KWELI. - MUNGU ni HAKIKA. - MUNGU Yu HAI.
Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.