DARASA/KONA YA MAFUNDISHO: ''Mkalimani Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY. (Darasa linaendelea pale lilipoishia jana,...) Yohana 8:32 “Tena mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru”. Unapofahamu ukweli wa jambo unapata Uponyaji, Ufumbuzi. Ni mambo mengi yamekusibu na yamekutesa na kukukandamiza kwa muda mrefu; ni vizuri ufahamu sasa kiini cha tatizo, kiini cha jambo ili ufikie mahali pa kutambua na kupona. Unapoenda hospitali hata kama umezidiwa sana, wanaweza wakakuwekea dripu za maji au dawa za kupunguza maumivu wakilenga kukusaidia upate muda kidogo ili waweze kutambua kiini cha tatizo; baadae watachukua vipimo labda damu, choo, mkojo, n.k na wakishagundua tatizo ni nini basi inakuwa rahisi kushughulikia hilo tatizo basi na huo unakuwa ndio uponyaji wako. Tatizo lisipogundulika,unaweza ukafa mapema. Kwa nini watu wa UKIMWI wanakufa mapema? Kwa sababu hawajatambua tatizo ni nini, wanaona tu matokeo yanayotokea mwilini na hatimaye kufa.; lakini malaria wameweza kuyashinda kwa sababu wametambua kiini chake ni mbu; na wale wadudu wanaosababisha wanawashughulikia kwa kuwaua na kuwapa wagonjwa dawa za kumaliza wale wadudu kulingana na wingi na aina zao. Mwanzo 3: 17-19 “Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako, michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa, kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi. Ujumbe huu unatupatia kujua mwanzo au asili ya laana ni dhambi yaani kutosikiliza maagizo ya BWANA MUNGU WETU.

KIBALI: Kuwepo kwetu Duniani ni KIBALI toka kwa MUNGU. Kuzaliwa kwako kwa kupitia tumbo la huyo Mama na kiuno cha huyo Baba ni KIBALI. MUNGU ALIWARIDHIA wao wakuzae Wewe, kwa njia gani, kwa namna gani MUNGU Anajua. Ulizaliwaje liwaje ISIKUSUMBUE, kwamba walikuwa na Dini, Imani MUNGU Aliwaridhia, MBEGU ilitoka ikaingia ukatokea. Kuna watu wanafanya uasherati toka asubuhi hadi usiku, wengine wameoana na watakatifu lakini hawajapata Mtoto; Ila Wewe ULIZALIWA,....: Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY, sehemu ya Mahubiri ya Jumapili jana tarehe 26/Jan/2014; (Mahubiri kamili yatapatikana kwenye Website yetu www.efathaministry.org, na kwenye Youtube yetu www.youtube.com/efathaministry pamoja na kwenye Blog yetu www.efathaministrypage.blogspot.com, Mbarikiwe wana wa MUNGU).

SHUHUDA ZA JUMAPILI YA TAREHE 26th JANUARY 2014 Mungu wetu ni mkuu sana, Mungu wetu ametukubali kwani tumepata kibali na watumishi wa Mungu kama wanavyo onekana mioyo yao inashukrani na wengi wao wamepata watoto wengine watoto wao walikuwa wanaumwa tangu kuzaliwa kwao lakini sasa hivi wana moyo wa shukrani Binti yao anatembea pia kuna Mtumishi wa Mungu anamshukuru Mungu kwani anamiaka 10 ya wokovu miaka 7 ya utumishi na miaka 6 ya ndoa hawana zaidi ya kumpatia Mungu zaidi ya Kumshukuru Mungu. “Mungu hana Upendeleo” Mungu hajakuacha na wewe msongeree naye atakupa KIBALI AMIN!!

Kelele haiji ulizaliwa vipi, inakuja unamalizia vipi Safari yako ya kuishi. Kwamba baba yako anaitwa nani haikusaidii. Vyovyote ulivyozaliwa isikusumbue (kwamba mama yako alibakwa, alidanganywa, chipsi zilizasababisha, lifti ilisababisha, iwe stendi ya basi n.k., vyote visikusumbue), la msingi angalia jinsi gani UNAVYOSONGA MBELE. Hakuna hata mmoja atakayetaka azaliwe na nani. BABA wa Mbinguni ndiye Asili ya kuzaliwa kwetu. ASILI yako wewe ni MUNGU, ndio maana wewe ni MALI YA MUNGU.: Apostle & Prophet Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Haijalishi Umezaliwa katika Mazingira gani, maadamu Wewe UMEOKOKA, UMEMKUBALI YESU KRISTO kuwa BWANA na MWOKOZI wa Maisha yako, ..... MSIKIE Mama huyu na Mwanae: Kipindi huduma hii ya MUNGU Wetu MKUU EFATHA MINISTRY inaanza pale Sinza, huyu mama alikuwa anatembea na kandambili tena zimechoka huku akiwa hoi taabani kimaisha akiuza MCHICHA Mchicha mitaani. Mtumishi wa MUNGU Mbeba Kusudi Mkalimani wetu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alikutana naye, naye Mama AKAMPOKEA YESU KRISTO Awe BWANA na MWOKOZI wa Maisha yake, baada ya Kuokoka akawa Anaendelea na Biashara yake ya Mchicha Mchicha, Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Akawa anamwombea, akawa anamwombea Mchicha UISHE Haraka ili awe anakuja kwenye MAOMBI, Na KWELI ilikuwa haichukui muda Mchicha mtaa wa kwanza, wa Pili UMEISHA, Hakuwa anachukua muda tena kutembea JUANI kwani Mchicha ulikuwa unamalizika mara moja kwa haraka sana. Mama huyu akawa anaendelea na Biashara yake LAKINI Sasa Akafikia wakati akawa na Vijana WANAMLIMIA na Yeye anaenda kuuza tu, Haleluyaaa...., SASA LEO HII Mwanae huyu (Pichani) AMEMALIZA ELIMU ya Chuo KIkuu''DEGREE''. Yule yule Mama Mchicha Mchicha aliyekuwa anatembea Juani, kandambili zimechoka, Maisha magumu taabani LEO SI YEYE TENA na MWANAE ANA DEGREE...Ndipo UONE Jinsi Gani MUNGU WETU ALIVYO MZURI, Uone jinsi gani YESU ALIVYO MZURIIII, Unataka Nini TENA? MWAMINI YESU, MPOKEE YESU, TULIA KWA MKALIMANI WAKO na MSIKILIZE VIZURI na ELEWA ANAKUAMBIA NINI... EFATHA ''FUNGUKA''. Ooooooh Haleluyaaaaaa Asante YESU, Asante YESU, Asante YESU, Tunakupenda BWANA, Tunakupenda YESUUU, Wewe ni MZURI YESU, Wewe ni MZURI, UNATUPENDA Wanao, Asante Nasi TUNAKUPENDA.

SHUHUDA SHUHUDA SHUHUDA: ASTELIA CHILAMBO, ZONE YA MBEZI BEACH B’ Anamshukuru MUNGU kwa kumponya mateso ambayo alikuwa anayapata kwa kuumwa mara kwa mara, kwa muda mrefu alikuwa akiteseka kwa magonjwa alikuwa akienda shuleni mama yake alikuwa anapigiwa simu kuwa mwanae anaumwa, mara nyingine ata usiku wa manane, mateso haya yalikuwa ni kawaida kwake toka baba yake alipofariki mwka 2007 (Wanasema baba yake alikuwa anampenda sana). Jumapili moja alikuja Kanisani Ibadani, akapata Neema ya kukutana na Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii, Mtumishi wa MUNGU akamwambia achemshe maziwa na anywe kwani alikuwa hanywi maziwa kutokana na vidonda vya tumbo, akanywa maziwa, baada ya hapo Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii alimpa maji na kumuambia anywe kidogo kidogo, HALELUYA UTUKUFU KWA MUNGU WETU JUU, toka hapo akawa amepona kabisa. Baada ya hapo alirudi shuleni lakini akawa anawaza sana kuhusu Mitihani kwani kabla ya Kuombewa na Mtumishi wa MUNGU alikuwa ana kipindi hajahudhuria masomo shuleni, kwa hiyo alikuwa anawaza kuhusu atafanyaje mitihani, lakini akamuomba MUNGU somo la Chemistry aweze kufaulu, HALELUYA MUNGU WETU NI MZURI, MUNGU wetu Alifanya Matendo yake MAKUU Astelia akawa wa kwanza katika Shule zote walizo kuwa wakishindanishwa katika hilo Somo la Chemistry. HALELUYA sasa Astelia Ni MZIMA wa Afya Njema na Anafanya VIZURI katika Masomo yake, SIFA KWA BWANA WETU YESU KRISTO ALIYE HAI ALFA na OMEGA, Asante YESU BWANA kwa KUTUPENDA SANA na Ukatupa KUSUDI HILI (EFATHA: Uponyaji na Ukombozi, Watu WAWEKWE HURU), Asante YESU, Tunakupenda BWANA, Asante. (Na Wewe uko unayeteseka, Jua KWAMBA YESU Anakupenda sana, YESU Anakuambia NJOO SASA, Naye ATAKUWEKA HURU, ANAKUPENDA, Njoo kwa YESU)

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.