USHUHUDA:
Naitwa Elizabeth Shabani kutoka Mkoa wa Tanga, Namshukuru Mungu kwa ajili ya Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira kwa kutulea vyema sisi wana Efatha. Mwaka 2012 nilikuja katika Kusanyiko na nilipofika katika kusanyiko hilo nilipokea Neno ambalo lilinifungua. Tulipokuwa katika Ibada Mtumishi wa Mungu akasema "kuna watu hapa ndoa zao zinamatatizo na wanataka kuachana", mimi nilikuwa ni mmoja wao.
Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii akasema nakataa kuachana katika Jina la Yesu, na wakati huo mimi nilikuwa nimekosana na mume wangu. Lakini nilimshangaa Mungu niliporudi nyumbani mume wangu alinifurahia na Upendo ukarudi, na mwaka huu mwezi wa saba ameokoka.
Katika kusanyiko hilo pia Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira akasema, wengine wanafanya biashara haziendi lakini sasa watafanikiwa, na wale wote wanaoishi kwenye nyumba za kupanga wakifika wakafukuzwe ili wakajenge za kwao, na walio na viwanja wakajenge. Neno hilo lilitimia kwangu kwani tulifukuzwa katika nyumba tuliyokuwa tumepanga. Sasa tunamshukuru Mungu kwani alitupa pesa ya kujenga nyumba ambayo tunakaa na tumepangisha wapangaji wawili. Namshukuru sana Mungu kwa matendo yake makuu aliyo nitendea katika Kusanyiko Kuu la Mwaka 2012 sifa na Utukufu anastahili Mungu wangu.
Ukisikia Neno kutoka kwa Watumishi wa Mungu ambalo linakuhusu shika hilo Neno mpaka litimie kwako, kwangu imekuwa naamini hata kwako itakuwa.

Comments