KUSANYIKO KUU LA TISA PRECIOUS CENTER KIBAHA.


SOMO: NEEMA.

Neema itakukumbusha wewe kuwa, pasipo Nguvu ya Mungu huwezi kufurahia wokovu wako.
Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.”
Wanafunzi wa Yesu walipo muomba Bwana Yesu awafundishe jinsi ya kuomba kama wanafunzi wa Yohana Mbatizaji, Bwana Yesu akawaambia “Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye Mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, ”

Bwana Yesu alikuwa hataki waombe kama wao, kwa sababu wao walikuwa mtu akiwa na pepo, alikuwa anapigwa mawe mpaka afe. Kwa wanafunzi wake alitaka iwe tofauti kwamba watakwenda kuwafungua na si kuwaua, kwa sababu Neema ilikuwa imewajilia.

Mathayo 6:9-10 “Ufalme wako uje hapa duniani” hakumaanisha kuwa Kiti cha Mungu kiwe huku duniani la! bali alitaka Akili ya Mungu iwe huku duniani na watu walioko huku waujue ule uumbaji, maana yake na kusudi lake. Na wakisha ipata hiyo mamlaka ndipo wataichukua hiyo mamlaka na kuitumia huku duniani. Hii ndiyo maana ya ile sala ya Bwana.

Bwana Yesu alitaka sisi tutambue kuwa aliye Mbinguni ni mmiliki wa kila kitu na ili tutambue kuwa sisi ni warithi pamoja na Mungu. Na chochote kinachotembea au ambacho kipo Duniani ni cha Baba yetu wa Mbinguni na ni chetu pia, na sisi ni wamiliki pamoja naye.

MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

Comments