KUSANYIKO KUU LA TISA
PRECIOUS CENTER KIBAHA SIKU YA TANO.
ASKOFU: CHARLES KARIUKI KUTOKA KENYA
Mungu wetu ni muwekezaji anaishi Mbinguni lakini anawekeza huku duniani. Huwezi kuheshimika katika nchi yoyote mpaka utakapo onyesha utajiri wako. Mungu anapojiongelea yeye mwenyewe Mungu ni muumbaji lakini haachi kuongelea utajili wake. Anasema Mbingu ni mali yangu, na vyote vilivyo katika nchi pia ni vyangu, na kisha anasema hata wanyama ni wangu pia.Anaiongelea dunia katika ile lugha Utakayo ielewa, ya kwamba yeye ni mmiliki wa kila kitu huku Duniani.
Roho yako lazima iwe na Nguvu ya kiuchumi, kwa sababu dunia hii ni ya kiuchumi na Mungu anaelewa, na wewe kama Mwana wa Mungu Unatakiwa uishi katika huo Utajiri.
Fedha ina kinywa, masikio na macho, lazima uiongeleshe fedha yako kwa sababu biblia inasema fedha ni jawabu la mambo yote. Kama fedha ni jawabu la mambo yote inamaana kuwa unapaswa kuiamrisha ikujilie hiyo fedha na si ikuamrishe wewe.
Si mapenzi ya Mungu wewe ufe maskini kwa sababu umaskini si wa Ufalme wa Mungu na hauna Utukufu, na Mungu wetu ni Mungu wa Utukufu. Kabla hujakwenda (Mbinguni) Mungu anataka wewe ufanikiwe na kumiliki hapa duniani kwanza (yaani utawale).

Comments