KUSANYIKO KUU LA TISA PRECIOUS CENTER KIBAHA SIKU YA NNE:
SOMO: NEEMA YA MUNGU:
Ibada ni nini? Ni ule uwezo wa mtu kumshukuru Mungu, watu wengi wanafikiri kumwabudu Mungu ni kumuomba mahitaji yao la! Kuabudu au Ibada ni tofauti, unapo jitiisha wewe mwenyewe kwa yule ambaye unafikiri kuwa ni mkuu kuliko wewe hiyo ndiyo inaitwa Ibada, pia kutoa dhabihu, ya mali na muda wako. Penye Ibada ya Mungu utaikuta Neema na Moyo wa Shukurani.
Kuna baadhi ya watu wanakuja Kanisani kila siku lakini wapo vile vile, huwezi kuona UTUKUFU kwao, KUONGEZEKA wala MSAADA wa MUNGU, kwa nini? Kwa sababu Roho wa Shauri hajaanza kazi ndani yao ili kuwafanya wawe watu wa Ibada.
Mungu hutafuta watu wale ambao wako tayari kumwabudu au kuwa na Ibada naye. Utawezaje kumfanyia Mungu ibada? Kwa kuwa na moyo safi, Roho wa Shauri itakusaidia wewe kujinyenyekesha mbele za Mungu ili uweze kufikia toba. Ukisha fikia toba ndipo sasa Mungu atakusikia kwa sababu utakuwa na ibada naye.
Roho ya Shauri atakuongoza namna ya kuipata toba, ukiwa katika maombi yenye Toba, kwa sababu unaongozwa na Roho, hofu ya Bwana itakushika na kukufanya uwe mnyenyekevu na mwenye moyo wa kupondeka mbele zake.

Comments