KUSANYIKO KUU LA TISA PRECIOUS CENTER KIBAHA.
SOMO: NEEMA.
Bwana Yesu alitaka sisi tuwe na Ufahamu wa ki-Mungu, akasema tangu enzi za Yohana Mbatizaji hata sasa Ufalme wa Mungu unapatikana kwa Nguvu. Ina maana kuwa tangu enzi za Nuhu mpaka Yohana Mbatizaji Wokovu wa Mungu ulikuwa unapatikana kwa Neema na ni mpaka Mungu akuridhie. Ila sasa Mungu ana achilia Neema yake kwa watu ili wafanye kazi yake. Kabla ya Yohana Mbatizaji Neema ilikuwa inakaa na Mungu mpaka aridhie kumpa mtu.
Baada ya Yohana Mbatizaji Mungu aliachilia Neema yake kwa kila mtu huku Duniani. Tangu enzi za Yohana Mbatizaji mpaka sasa waabuduo halisi ndio wale ambao wana sababisha Mungu asikae kimya. Malaika wanahangaika kuwahudumia ili Ibilisi apate shida. Unapompenda Mungu na kumfurahia yeye unamfanya anachanganyikiwa kwa ajili yako. Ufalme wa Mungu unapatikana kwa nguvu. Ni kwa nguvu tu ndipo unaweza kuupata Ufalme wa Mungu

Comments