KUSANYIKO KUU LA TISA PRECIOUS CENTER KIBAHA.
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA:
SOMO: NGUVU ZA MUNGU:
Katika uwepo wa Nguvu ya Mungu kuna USHINDI, ukiwezeshwa na nguvu hii wakati wengine wanashindwa wewe hutakaa ushindwe na chochote kile.
Wafilipi 4:13 “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” Kama una Nguvu ya Mungu chochote kitakachokuja katika akili yako hakuna atakaye thubutu kukuzuia.
Nguvu ya Mungu inakutoa mahali pa chini na kukupeleka mahali pa juu.
Neema itakufundisha namna ya kuipokea Nguvu ya Mungu na pia itakupa kuona faida katika maisha yako. Neema itakukumbusha kuona kuwa bila Nguvu ya Mungu huwezi kufurahia maisha.

Comments