KUSANYIKO KUU LA TISA, EFATHA MINISTRY PRECIOUS CENTER KIBAHA:
ASKOFU: CHALRES KARIUKI - KUTOKA KENYA
Marko 4:35 “Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo. ” Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake na tuvuke ng’ambo.
Kule Upande wa pili, Upande wa ng’ambo ni wa Ushindi, hakuna kushindwa bali ni upande wa kushinda.
Mungu akamwambia Musa wewe uko ukingoni mwa Bahari, hawa watu wa Ibrahimu lazima waivuke hiyo Bahari ya Shamu mpaka ng’ambo ili waweze kurithi. Musa aliwaongoza wana wa Israel kuelekea nchi ya Ahadi. Wale ambao ulikuwa ni uzao mchanga walikuwa ni uzao wa Yoshua na Kalebu, lakini uzao uliotoka Misri ulikufa jangwani. Hivyo ilimbidi Musa na yeye afe ili ule uzao mchanga uweze kufika katika nchi ya Ahadi.

Yoshua 12:7 “Hawa ni wafalme wa hiyo nchi ambao Yoshua na wana wa Israeli waliwapiga ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa magharibi, .... ”
Walipokuwa ng’ambo ya Yordani Musa aliwapiga wafalme wawili, Sihoni mfalme wa Waamori na Ogu Mfalme wa Bashani ili kumuonyesha Yoshua njia na ili kumfundisha Yoshua kuwa si yeye atakaye wapigania Israel watakapo vuka Yordani bali ni Mungu. Upande wapili wa mto Yordani kulikuwa kuna vitu vingi vya kumiliki.
Baada ya kuvuka Yordan nchi ya kwanza kuweza kuimiliki ni Yeriko maana ilikuwa imefungwa, lakini Mungu aliwapa kuimiliki kwani aliwawezesha wao kuingia ndani. Upande wa ng’ambo kuna adui wamekalia Mbaraka wako lakini utakapovuka usihofu kwa sababu upande wa ng’ambo Mungu atakufanya Ustawi, kwa sababu chochote kile ambacho adui yako amekalia ni cha kwako.

Comments