ASKOFU CHARLES KARIUKI KUTOKA KENYA:

SOMO: WEWE NI NANI NA MUNGU AMEWEKA NINI NDANI YAKO

Mungu alipo muumba mwanadamu alimbariki, ili akawe na mamlaka ya kutawala kila eneo la nchi maana ndiyo milki yake. Mamlaka yako haipo tu kwenye nyumba yako, bali hata katika anga lako na kitu chochote kile kilicho katika nchi kipo katika milki yako.

Hapa duniani Mungu aliukabidhi wajibu wa kumiliki au kutawala kwa wanadamu, na alipotoa hiyo mamlaka Mungu akaacha kufanya kazi. Si kwamba Mungu alichoka bali ni kwa sababu kazi yake aliikabidhi kwa mwanadamu.
Mungu wetu si Mungu wa kuchanganya mambo kwa sababu yeye ni Mungu wa mipangilio na anapo kukabidhi kitu wewe, hawezi kuja kukuingilia anakupa uhuru kamili katika kitu hicho.

Sisi ni watawala, hivyo Mungu alipo muumba mwanadamu ilibidi amjaribishe kwanza kama uumbaji wake upo kwa huyo mwanadamu. Hivyo Mungu aliwaumba wanyama na kumletea Adamu ili awapatie majina. Mungu alipo ona kuwa Adamu ndani yake kuna uumbaji baada ya kuwapa majina wanyama wote, akajua kuwa pia kuna Utawala ndani ya Adamu. Na ndio maana hata baada ya Mungu kumuumba mwanamke alimpa Adamu ili ampe jina.

Comments