ASKOFU CHARLES KARIUKI KUTOKA KENYA:
SOMO: UBABA.
Baba ni msingi, chanzo na muendelezo, na Baba ndiye anayeleta Ubaadae wa mtu. Mtu anayeleta hitimisho la kusudi kwa mwingine ni Baba, kwa sababu kutokana na Baba ndiyo tunaweza kutengeneza familia.
Unapokuwa na Baba una ubaadae, ukitaka kujua ubaadae wako muangalie baba yako.
Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira ni Baba yetu, hivyo tunaweza kujua ubaadae wetu unafanana je kwa kumtazama yeye kama Baba yetu. Kama Baba yetu hajashindwa basi na sisi hatutashindwa. Imani yetu inapaswa kuunganika na chanzo chetu, yaani Baba yetu.
Wanafunzi wa Ibrahimu walimuelewa sana Baba yao kuliko hata Bwana Yesu.

Mungu wetu wa Mbinguni yeye ni MWENYE NGUVU, ana KILA KITU na ndiye Muumbaji wa MBINGU na NCHI lakini katika vyote alivyo vifanya alichagua cheo kimoja juu ya vyeo vyote, ambacho ni CHEO CHA UBABA. Mungu BABA yeye ndiye chanzo, msingi na muendelezo. Hapa duniani Mungu anatenda kazi kupitia ma Baba na si wazazi, maana katika Dunia hii ma Baba ni wachache lakini wazazi ni wengi. Hivyo kama huuelewi Ubaba hutaweza kumuelewa Mungu wala hutaweza kuelewa ile mamlaka aliyo ishusha katika Kanisa.

Comments