ZIARA YA KITUME NA KINABII MKOA WA KIGOMA.
SOMO: NEEMA YA BWANA YESU.

NEEMA ni ya MUHIMU sana katika Maisha ya kila mtu huku duniani.
Yohana 15:5 “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya NENO lo lote.” Pasipo Neema hakuna kitu kitakachoendelea katika Maisha yako. Ukiwa na IMANI bila NEEMA itakupa kwenda MBINGUNI lakini hutaweza KUZAA MATUNDA na Maisha yako yatakuwa ni ya kawaida tu huku duniani.


Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.” (Ninyi mkikaa ndani yangu) ina maana kuwa wewe ukikaa ndani ya hiyo NEEMA, ambayo ni “Bwana YESU” omba lolote nawe utapewa, NEEMA ni ya muhimu sana kwako kama unataka KUSTAWI na KUCHANUA.

Ni katika NEEMA ndipo unaweza KUPANDISHWA daraja la KIROHO bila NEEMA utaishi maisha ya UCHANGA wa KIROHO kila iitwapo leo.
Pasipo NEEMA huwezi kuwa mwanafunzi maana hata ukifundishwa hutakuwa unaelewa.

Ni katika NEEMA tu ndipo unaweza Kumtukuza na Kumpendeza Mungu, pasipo NEEMA huwezi Kumpendeza MUUMBA wako.
Ni katika NEEMA tu ndipo unaweza kumshinda shetani, nje ya ATAKUBURUZA.

MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA, EFATHA MINISTRY.


Comments