SOMO: SALA YA BWANA.
Mathayo 6:9 “Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, ”
“Kwa kuwa Ufalme ni wako na Nguvu na Utukufu hata milele Amen.”
Biblia inasema ombeni kwa Baba yenu wa Mbinguni si kwa Malaika, Watakatifu waliopo Duniani au Mbinguni, Hapana. Bwana YESU alitufundisha sisi kwa sababu ni wake na YEYE alituchagua ili tuwe wake na tumekubaliwa, hivyo Baba wa Minguni ametukubali ili tuwe Wana kwake. Hatuhitaji kuomba kupitia kwa (niaba) mtu fulani bali tunapaswa kwenda moja kwa moja kwa Mungu kwani tumeruhusiwa, na Bwana YESU ametuambia tuombe kwa JINA lake nasi tutapewa.
UFALME wako uje; Ufalme wa Mungu unakuja pale Mapenzi ya Mungu yanapokuja ndani yako, na unapotenda sawasawa ndipo UFALME utakapokujilia ndani yako.
Kuna mambo unahitaji kufanya ili usababishe au uruhusu UFALME ukujilie, ule UTUKUFU wa Mungu Mkuu huwa unakuja pale Nguvu na Utukufu zinapojidhihirisha kwako.
Mathayo 7:18 “Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.” Yeyote asiyeweza kufanya mapenzi ya Mungu hawezi kuchochea Nguvu ya Mungu ndani yake na wala Nguvu ya Mungu haiwezi kuweka Makao ndani yake. Hivyo kama wewe ni muovu, haufanyi Mapenzi ya Mungu sahau WEMA wa Mungu kuja kwako, utawasikia watu wakisema au wakishuhudia, lakini kwako wewe watu wataona ukilia na ukinung’unika na kulalamika. Kwa nini? Kwa sababu hauyatendi Mapenzi ya Mungu. Fanya mambo sawasawa na Mapenzi ya Mungu ili uweze kupokea vilivyo vya Kwake.

Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira - EFATHA MINISTRY.


Comments