SOMO : NGUVU YA MEMA NA MABAYA.
MUNGU ni ROHO haonekani kwa macho haya ya damu na nyama, ni NEEMA Kama ukijaliwa kuona mambo ya MUNGU au WEMA wa MUNGU hata ukafikia hatua ya KUAMINI.
Tunamjuaje MUNGU? Tunamjua MUNGU kupitia MATENDO yake, Matendo ndiyo yanayotupa kutambua aliyefanya jambo ni MUNGU au LA!. Kuna mambo yakifanyika kila mmoja anasema, "Huyu aliyefanya haya ni MUNGU ". Pia kuna mambo ambayo yakifanyika unajua aliyefanya si MUNGU.
Ni kwa NEEMA tu ndipo tunaweza Kumjua MUNGU na Kumwamini, pasipo NEEMA ni ngumu kupambanua mambo ya MUNGU.
:- Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira - EFATHA MINISTRY.

Comments