SOMO: NEEMA YA BWANA YESU.

ZIARA RA KITUME NA KINABII MKOA WA KIGOMA.
SOMO: NEEMA YA BWANA YESU.

NEEMA inakupa Nguvu ya kushinda dhambi, Warumi 7:14 “Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya Rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.” Ukiwa na NEEMA utaweza kuishinda dhambi, itafute NEEMA itakusaidia kukufikisha mahali pa FARAJA yako. 
Ni NEEMA tu ndiyo inayosababisha Akili yako iweze kumtumikia Mungu, maana bila NEEMA itakuwa inawaza dhambi tu, ukiwa na NEEMA itaifundisha akili yako jinsi ya kumtumikia Mungu. 

Ukiwa na NEEMA ndio utaweza kuwa BORA kuliko wengine,
Neema isipokuwepo hata lugha yako inakuwa mbaya, na hata maisha yako yanakuwa yamebana, ukiona maisha yamebana jua kuwa NEEMA imepungua au haipo kabisa, lakini maisha yanapoanza kuwa nafuu jua kuwa Neema imeanza kutokea kwako. 

Pokea hiyo NEEMA uende nayo katika Maisha yako, Kazi zako na Biashara zako ili ikufundishe kupata Faida, kwa JINA la YESU, Amen.

:- Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, EFATHA MINISTRY.

Comments